Saturday May 25, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

`Vijana Msalaba Mwekundu jiepushe na rushwa`

9th May 2012
Print
Comments

Vijana wa Chama cha Msalaba Mwekundu nchini wametakiwa kufanya kazi yao kwa uadilifu na kuepuka kuchukua rushwa wakati  wakisaidia wahanga kwani ni jukumu lao kuwasaidia.

Hayo yamesemwa jana jijini Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Dk. Zainab Gama, wakati wa maadhimisho ya siku ya Msalaba Mwekundu duniani yenye kaulimbiu ‘Vijana katika mwendo’.

Gama alisema chama hicho pia kimezindua kampeni ya kitaifa ya kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu matumizi sahihi ya nembo ya Msalaba Mwekundu. “Kampeni hii itaenda sambamba na na mchakato wa kurekebisha sheria ya mwaka 1962 namba 71, iliyoanzisha chama ili iendane na mazingira ya sasa,’’ alisema Gama.

Aidha, aliwataka wadau mbalimbali kukusaidia chama hicho ili kiweze kufanya kazi yake kwa ufasaha na kwa wakati.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment