Saturday Apr 30, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Yanga kusaka mchawi J`mosi

26th April 2012
Print
Comments

Kamati ya Utendaji ya Yanga inatarajia kukutana keshokutwa katika kikao cha dharura ili kujadili hali ya 'ndivyo sivyo' iliyopo ndani ya klabu yao kufuatia matokeo mabaya yaliyowatoa katika mbio za kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Moja ya agenda inayotarajiwa kuzungumzwa kwenye kikao hicho ni kuhusiana na uzembe uliofanyika wa kumchezesha beki Nadir Haroub 'Cannavaro' katika mechi waliyoshinda 1-0 dhidi ya Coastal Union na kusababisha wapokonywe pointi kwani beki huyo alikuwa akitumikia adhabu ya kukosa mechi tatu.

Kikao hicho pia kitazungumzia hali ya ukata ambao unaikabili klabu hiyo, hali ambayo inadaiwa kuwa imechangia kushusha morari ya wachezaji kuelekea mwishonni mwa msimu.

Akizungumza juzi usiku kwenye mahojiano na redio moja nchini, Mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga, alisema kuwa Kamati ya Utendaji itakutana keshokutwa (Jumamosi) kujadili mambo mbalimbali yaliyojitokeza kwenye klabu yao.

Nchunga alisema kuwa licha ya kupoteza ubingwa wao, wanafahamu kwamba klabu yao inakabiliwa na mechi ya kukamilisha msimu dhidi ya watani zao wa jadi, Simba, ambayo itachezwa Mei 5 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Baada ya kupoteza ubingwa na nafasi ya kushiriki kwenye mashindano ya kimataifa mwakani, Yanga pia imepata pigo jingine kufuatia viongozi wake wawili muhimu kujiuzulu nafasi zao.

Viongozi hao ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Seif Ahmed ‘Magari’ na Abdallah Bin Kleb waliotangaza kujiuzulu, huku mjumbe mwingine, Theonest Rutashoborwa, akifariki dunia.

Imeelezwa kuwa Magari na Bin Kleb waliamua kujiuzulu baada ya kuona kuwa wanakosa ushirikiano wa kutosha kutoka kwa baadji ya viongozi wakuu na hivyo kuzifanya kamati walizokuwa wakizitumikia kushindwa kutekeleza vyema majukumu yake.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles