Wednesday May 4, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Viwanda vidogo vinasaidia ajira:Dk Shein

28th April 2012
Print
Comments
Rais wa Zanzibar DK Ali Mohamed Shein

Rais wa Zanzibar DK Ali Mohamed Shein, amesema kwamba viwanda vidogo vidogo vina nafasi kubwa ya kupunguza tatizo la ajira kwa wananchi wake.

Dk Shein alisema hayo baada ya kuzindua kiwanda  cha kutengeneza sabuni cha ‘Mkipi Spice Soap’ kinachomilikiwa na ushirika  wa Mkipi katika Wilaya ya Wete Kisiwani Pemba.

Alisema kwamba kiwanda hicho kitasadia kuongeza ajira na kufanikisha mpango wa serikali wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini kwa wananchi wake.

Hata hivyo, aliutaka uongozi wa kiwanda hicho kuhakikisha bidhaa wanazotegeneza wanazitangaza katika soko la ndani la Zanzibar na Tanzania Bara.

“Jambo la msingi tumieni vyombo vya habari kutangaza bidhaa zenu katika soko la  Zanzibar na Tanzania Bara,” alisema Dk Shein.

Kwa upande wake, Waziri wa Biashara Viwanda na Msoko Nassor Ahmed Mazrui, alisema kwamba serikali imeamua kuimarisha Sera ya Viwanda kutokana na sekta hiyo kuwa na mchango mkubwa katika kuharakisha maendeleo ya Zanzibar na wananchi wake.

Waziri Mazrui alisema kwamba serikali itaendelea kufanyakazi kwa karibu na wajasiriamali na tayari imeanzisha utaratibu wa kuwapatia mafunzo nje ya nchi ili bidhaa kuwajengea uwezo kutengeneza bidhaa zenye kiwango cha ubora.

Alisema kiwanda hicho kimefanikiwa kupata msaada wa mashine kutoka Shirika la maendeleo la misaada la Marekani (USADF),  wenye thamani ya  zaidi ya Sh Milioni 13.

Awali fundi wa kiwanda cha Sabuni cha Mkipi Seif Salim Seif,  alisema kwamba kiwanda hicho kimekuwa kikitengeneza sabuni za kuogea na kufulia kwa kutumia malighafi za Karafuu, mafuta ya makonyo, pamoja na mafuta ya Nazi.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles