Thursday May 5, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Malawi watua

25th May 2012
Print
Comments
Timu ya Taifa ya Malawi

Wakati timu ya taifa ya Malawi iliwasili nchini jana ikiwa na wachezaji 28, kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen, ameleezea kukoshwa na viwango vya wachezaji Mbwana Samata wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Mwinyi Kazimoto wa Simba katika mazoezi ya timu hiyo ya kujiandaa kuivaa Malawi kesho.

Kim alisifu viwango vya Samata na Mwinyi akisema ni watu unaoweza kuwategemea kubadilisha matokeo.

Mchezaji mwingine alionyesha kung'aa kwenye kikosi hicho ni beki Shomary Kapombe wa Simba huku yosso Ramadhani Singano 'Messi' (Simba), Frank Domayo (JKT Ruvu), Edward Christopher (Simba) na Salum Aboubakar wa Azam wakionekana kufanya vizuri na kuwa makini kusikiliza kile wanachoambiwa na kocha huyo aliyechukua mikoba ya Jan Poulsen.

Nyota wengine wa timu hiyo, Haruna Moshi 'Boban', Mrisho Ngassa na John Bocco, nao wanaonekana kupambana kwenye mazoezi hayo ili kujihakikishia namba katika kikosi cha kwanza.

Nahodha wa timu hiyo, Juma Kaseja, aliliambia gazeti hili kuwa wachezaji wote wako vizuri na kila mmoja ana ndoto za kusaka ushindi ili kurejesha heshima.

Kaseja alisema kwamba kila mchezaji anafanya juhudi katika kukuza kiwango chake na hatimaye kuifanya timu iwe bora.

Mara baada ya mechi ya kesho dhidi ya Malawi, Taifa Stars Jumatano ya Mei 30 itasafiri kuelekea jijini Abdijan kuwavaa wenyeji Ivory Coast katika mchezo wa kusaka tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwaka 2014 huko Brazil.

Hata hivyo, katika mechi ya kesho Stars itawakosa wachezaji wawili, Nurdin Bakari na Thomas Ulimwengu ambao wameumia wakiwa mazoezini.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles