Saturday Apr 30, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Udhibiti wa matumizi ya Dola waanza

25th May 2012
Print
Comments
Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene

Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Benki Kuu (BoT) imeanza kufanya utafiti ili kudhibiti watu, makampuni na taasisi zinazopenda kufanya biashara kwa kupokea Dola ya Marekani badala ya kupokea fedha za ndani.

“Tumeanza utafiti kwa kushirikiana na BoT…tutaongea nao na kupanga utaratibu ili kuwataka wadau watumie fedha za ndani badala ya Dola katika biashara zao,” alisema Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene, baada ya kufungua semina kuhusu Masoko ya Fedha na Taasisi za Fedha.

Alisema sheria zilizopo haziruhusu watu au makampuni kufanya biashara kwa kutumia fedha za kigeni kwa sababu hatua hiyo inachangia kushusha thamani ya Shilingi.

“Hawa wafanyabiashara wetu wanapokea Dola na serikali haijui kiasi gani cha Dola  kimeingia,” alisema na kuongeza: “Uchumi wetu haujawa mbaya kiasi cha kuhitaji matumizi ya Dola katika biashara zetu.”

Alisema wafanyabiashara wanaweza kufanya mauzo kwa kiwango cha Dola,lakini wakapokea fedha za ndani badala ya fedha za nje.

Alisema baada ya utafiti huo, serikali itawasiliana na wadau kuhusu umuhimu wa kutumia fedha za ndani katika biashara zao ili kuifanya shilingi ya ndani iweze kuimarika na hivyo kuinua uchumi wa taifa.

Alitoa mfano wa Kenya, ambako alisema wananchi wake hawafanyi biashara kwa kutumia Dola za Marekani, na pale wanapotakiwa kuzipokea huwataka waende kwanza kuzibadilisha kwenye madua ya kubadilishia fedha.

Alisema tofauti na hapa, wafanyabiashara wengi wanapenda kupokea fedha za kigeni katika biashara zao hatua ambayo inaweza kuhatarisha thamani ya shilingi ya hapa.

Alitoa mfano wa Zimbabwe ambako matumizi ya Dola yalikuwa yamehalalishwa lakini yamefanya fedha yao kushuka thamani.
 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles