Sunday May 1, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Al Ahly watua leo kuivaa Simba

26th April 2012
Print
Comments
Kikosi cha Simba

Wapinzani wa Simba katika michuano ya Kombe la Shirikisho, klabu ya Al Ahly Shandy kutoka Sudan itatua nchini leo saa 7:00 mchana kwa ajili ya mechi yao ya awali ya hatua ya 16 bora itakayofanyika Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jana kwenye makao makuu ya klabu yake, Afisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema kuwa kikosi cha Al Ahly kinatarajiwa kuwasili na msafara wenye wachezaji 20 na viongozi 10, tayari kwa ajili ya mchezo wao wa kwanza wa michuano hiyo ya kimataifa.

Kamwaga alisema kuwa maandalizi ya mchezo huo yanaendelea na kwamba kikosi cha Simba kimeshaingia kambini rasmi juzi jioni kwa lengo la kujiweka 'fiti' kuwavaa wapinzani hao.

Alisema kwamba waamuzi wa mechi hiyo kutoka Swaziland na kamisaa ambaye anatoka Rwanda tayari wameshatumiwa tiketi za ndege na watatua nchini kesho.

Aliongeza kuwa tiketi za mechi hiyo ambazo kiingilio cha chini ni Sh. 5,000, zitaanza kuuzwa kesho kwenye vituo mbalimbali jijini na kusema kuwa pia kutakuwa na huduma maalum ya kuwapokea na kutenga tiketi za mashabiki wanaotoka mikoani ambao tayari wameshaanza kufanya mawasiliano na uongozi wa klabu hiyo.

"Pia tutapenda kuishukuru serikali kwa kutupa ruhusa ya kutumia Uwanja wa Taifa na kwa maana hiyo, tutajiandaa vizuri na tunaamini tutafanya vizuri kwa sababu, kiufundi Setif (ya Algeria) ilikuwa ndio timu ngumu ukilinganisha na Al Ahly Shandy tutakayocheza nayo Jumapili," Kamwaga aliongeza.

Alisema vilevile kuwa klabu yao inawaomba mashabiki na wanachama wao kuvaa nguo zenye rangi nyekundu na nyeupe na kuishangilia timu yao kuanzia dakika ya kwanza hadi mwisho wa mchezo.

Daktari wa Simba, Cosmas Kapinga, aliiambia NIPASHE kuwa beki Shomary Kapombe anaendelea vizuri na Jumapili atakuwa tayari kucheza kama kocha ataamua kumtumia.

Kapombe aliumia katika mechi yao ya Ligi Kuu ya Bara Jumapili iliyopita dhidi ya Moro United na nafasi yake ilichukuliwa na Nassoro Masoud 'Chollo' katika dakika ya 46 ya mechi hiyo.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles