Wednesday May 4, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Mkimbiaji Marwa kwenda Ujerumani leo

26th April 2012
Print
Comments

Mwanariadha Dickson Marwa anayekimbia mbio ndefu za Marathon ataondoka nchini leo kuelekea Hamburg, Ujerumani kushiriki michuano ya riadha ya kutafuta nafasi ya kufuzu michezo ya Olimpiki.

Mashindano hayo yanayoshirikisha wanariadha kutoka nchi tofauti duniani, yamepangwa kuanza April 29 nchini humo.

Akizungumza na NIPASHE jana, kocha wa mwanariadha huyo, Zacharia Gwandu, alisema maandalizi ya safari ya mwanariadha huyo anayetarajia kuiwakilisha nchi katika michezo ya Olimpiki imekamilika.

"Tayari tumepata tiketi ya Dickson ya kuelekea Ujeruman katika mashindano ya Marathon, nina imani atafanya vizuri ili apate nafasi ya kushiriki michezo ya Olimpiki," alisema Gwandu.

Gwandu alisema kuwa awali, sababu kubwa iliyokuwa ikiiweka shakani safari ya Marwa ni kuchelewa kwa tiketi yake.

Marwa aliiambia NIPASHE kuwa Watanzania wamuombee na anaamini kuwa atafanya vizuri kwani ameshafanya maandalizi ya kutosha ili afuzu kwa kushiriki katika michezo ya Olimpiki itakayofanyika Julai jijini London, England.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles