Saturday Apr 30, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Misri `yalipiga jeki` Jeshi la Polisi

3rd May 2012
Print
Comments
Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali, Saidi Mwema

Ubalozi wa Misri nchini umetoa msaada wa mashine ya huduma ya mionzi (X- Ray), yenye thamani ya Dola za Marekani 170,000, kwa Jeshi la Polisi kwa lengo la saidia huduma ya kitabibu.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya mashine hiyo, jana jijini Des Salaam, Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali, Saidi Mwema, alisema mashine hiyo itasaidia kuleta ushahidi wa kitabibu kwa wataalumu sambamba na wagonjwa kupata matibabu ya uhakika.

“Maishine hii itasaidia sana katika hospitali yetu ya polisi Kilwa Road pamoja na kuwarahisishia wataalumu matibabu watakayo mpatia mgonjwa kuwa stahiki,” alisema Mwema.

Alisema huduma ya mashine hiyo itasaidia askari polisi pamoja na wananchi hususani wanaozunguka maeneo hayo. “Kituo cha  afya cha barabara ya  kilwa kinatoa huduma kwa wananchi na pamoja na  askari polisi,” alisema Mwema na kuishukuru Misri kwa msaada kwa huo.

Balozi wa Misri nchini, Hossam Moharam, alisema msaada huo ya sio mwisho wa kuisaidia Tanzania bali itaendele kufanya hivyo kwa kuzingatia mahusiano mazuri yaliyopo.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles