Wednesday May 4, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Akutwa na mikia 12 ya tembo

29th April 2012
Print
Comments

Mkazi wa Mahenge, Wilaya ya Ulanga, Bonaventura Nahyoma (41), anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kupatikana na mikia 12 ya tembo.

Kaimu Kamanda wa Polisi Joseph Rugila, alisema ofisini kwake juzi kuwa tukio hilo lilitokea Aprili 24, mwaka huu, saa 5 asubuhi katika kijiji cha Karangayakero tarafa ya Mtimbira wilayani Ulanga mkoani hapa.

Kamanda alisema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa na nyara za serikali hizo kinyume na sheria na anatarajia kufikishwa mahakamani.

Wakati huo huo, mkazi wa Malinyi wilayani Ulanga mkoani hapa Anthony Luseba (30) anashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kukamatwa akimiliki silaha bila kibali.

Kamanda Rugila alisema kuwa tukio hilo lilitokea Aprili 26, mwaka huu majira ya saa 10 jioni katika tarafa ya Malinyi wilayani humo.

SOURCE: NIPASHE JUMAPILI
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles