Saturday Apr 30, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Tanzania katika kitisho cha magaidi

15th May 2012
Print
Comments
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ispekta Jenerali Said Mwema

Tanzania  ni miongoni mwa nchi zinazokabiliwa na vitisho vya vikundi vya kigaidi vya Al- Shabab na  Al-Qaeda pamoja na maharamia kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Somalia.

Tahadhari hiyo ilitolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ispekta Jenerali Said Mwema, wakati wa ufunguzi wa kikao cha siku mbili chenye lengo la kuimarisha ulinzi na ushirikiano kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO).

Mwenyekiti wa mkutano huo ni Kamishna wa Jeshi la Polisi kutoka Afrika Kusini, Luteni Jenerali Nhlanhla Mkhawanazi.

Hata hivyo, Mwema, alisema vitendo vya uhalifu mwaka 2010 hadi 2011 vimepungua kwa asilimia 19, japo changamoto ni nyingi zinazolikabili jeshi hilo.

“Matishio ni mengi sana kuhusiana na vikundi vya kigaidi vya Al- Qaeda na Al- Shabab mbali na kukabiliwa na maharamia katika ukanda wa Ziwa Tanganyika, Victoria na Bahari ya Hindi” alisema.

Aidha alisema, katika kika hicho watajadili mambo matatu aliyoyataja kuwa ni, kupata muongozo wa nafasi ya mwenyekiti wa jumuiya hiyo katika kikao kijacho kitatakachofanyika Afrika Kusini.

La pili  ni kuangalia uwezekano wa kusaidiana kiulinzi kwa lengo la kujiimarisha na kukabialiana na vitisho vya kigaidi.

Jambo la tatu ni kutazama masuala ya utekelezaji wa kikao kilichofanyika mwaka jana sambamba na mafanikio yake.

IGP Mwema, pia alisema kumekuwa na wimbi kubwa la vijana wa Kitanzania wanaokwenda Afrika Kusini kwa lengo la kutafuta maisha,  jambo linalopelekea kuishi katika nchi hiyo kama wahamiaji haramu.

Mbali na hayo, alieleza kuwa kikao hicho kitajadili namna ya kukabiliana na uhalifu kwa njia ya mitandao na ule wa uingizaji bidhaa hafifu na bandia katika soko.

Kwa upande wake Mwenyekiti SARPCCO, Luteni Jenerali Nhlanhla Mkhawanazi, alisema wapotayari kutoa ushirikiano kukabiliana na matukio ya kihalifu kwa lengo la kuimarisha ulinzi na kuwa na umoja.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles