Thursday Jun 20, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Wachezaji 19 Simba, Yanga ruksa kuhama

22nd June 2012
Print
Comments
Kikosi cha Simba

Wachezaji wanane wa klabu ya Simba na wengine 11 wa Yanga hawana mikataba na timu hizo na wako huru kufanya mazungumzo na klabu yoyote ndani na nje ya nchi, imefahamika.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Saad Kawemba, bila kutaja majina ya nyota hao alisema kuwa wachezaji hao walishamaliza mikataba na wanachotakiwa sasa ni kujipanga upya kujua watachezea wapi katika msimu ujao.

Kawemba alisema pia wachezaji wengine 12 wa Mtibwa Sugar ya Manungu, Turiani mkoani Morogoro nao mikataba yao imemalizika na endapo uongozi wa klabu hiyo hautawaongeza mkataba hawatavaa jezi ya timu hiyo msimu unaokuja.

Kawemba alizitaka klabu zote kuhakikisha zinafanya zoezi hilo la usajili kwa kufuata taratibu na kuzisisitiza zisikiuke makubaliano ambayo iliingia na wachezaji wake.

"Ni vyema kufuata taratibu, huu si wakati wa kufanya mambo yasiyokuwa na faida, ni vizuri wachezaji na viongozi wakakaa na kufuata taratibu zinazofahamika na hakuna kitakachoharibika," alisema kiongozi huyo.

Aliwataka pia wachezaji kuwa makini na mikataba wanayoingia na kuwapa tahadhari ya kutafuta washauri kabla ya kufanya maamuzi ili wasije kujuta hapo baadaye.

Mbali na kusajili nyota wapya, Simba na Yanga hivi sasa ziko katika mazungumzo na wachezaji wake wengine kwa nia ya kuvunja mikataba yao lakini kinacholeta 'utata' ni malipo kwa nyota hao waliopigiwa mstari mwekundu, ambao wanataka walipwe kwa mkupuo na si awamu tofauti na wanavyoombwa.

Pia wachezaji wengine wanakataa kupelekwa katika klabu nyingine kwa mkopo na wanasisitizwa walipwe fedha na wavunje mikataba iliyopo ili kila mmoja awe huru.

Hadi sasa beki Kelvin Yondani ndiye anayezigonganisha Simba na Yanga lakini mabingwa wa Kombe la Kagame ndio wenye nafasi kubwa ya kumtumia beki huyo anayekipiga pia kwenye timu ya taifa (Taifa Stars).


SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment