Monday May 2, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Wakili wa Mnyika ataka itaka mahaka imwachie huru

5th May 2012
Print
Comments
Wakili wa Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika

Wakili wa Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika, Edson Mbogoro ameiomba mahakama kumuachia mteja wake kwa kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuithibitishia mahakama kwa ushahidi mzito bila kuacha shaka katika madai yao.

Akitumia hukumu iliyompa ushindi Mbunge wa Segerea, Dk. Makongoro Mahanga, Mbogoro aliitaka mahakama kumuachia jimbo mteja wake.

Mbogoro alidai hayo jana mbele ya Jaji Upendo Msuya anayesikiliza kesi hiyo Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam wakati akifanya majumuisho ya mwisho baada ya pande zote mbili kumaliza kutoa ushahidi.

Alidai kuwa dosari ya kuzidi kwa kura zaidi ya 14,000 haina ubishi mahakamani kwani makosa yalifanyika hivyo waliiomba mahakama kutobatilisha matokeo kwa sababu hiyo badala yake wagawe kura zilizozidi kwa wagombea 16 waliokuwa wakigombea ubunge katika jimbo hilo.

Alidai kuwa hata kura 14858 zikigawanywa kwa wagombea 16 kila mgombea atapata kura 929 ambazo hazitamfikisha popote mdai, Hawa Ng'humbi na hata angepewa zote bado Mnyika angemzidi kwa kura 1440.

Alidai kuwa, mdai ameshindwa kuthibitisha madai aliyowasilisha mahakamani, na kuomba mahakama ione kwamba dosari zilizojitokeza hazikuathiri uchaguzi na matokeo yaliyompa ushindi Mnyika yalizingatia matakwa halali ya wananchi wa jimbo la ubungo.

Naye wakili wa Serikali Justus Mulokozi, akiwasilisha majumuisho yake alisema katika ushahidi uliotolewa na Ng’umbi bado hajui dosari za kura zaidi ya 14,000 ziliathiri vipi matokeo na kwamba hakuna uthibitisho kuwa hali hiyo iliathiri uchaguzi.

Alidai kuwa hata madai kwamba aliitwa fisadi, hayana uthibitisho na kwamba hali hiyo iliathiri vipi uchaguzi pia hakuna ushadi kwani hakuna mtu aliyefika mahakamani na kudai kuwa hakumpigia kura Ng’umbi kutokana na tuhuma za kushiriki kuuza jengo la UWT.

Aidha Mulokozi aliomba mahakama isitengue matokeo yaliyompa ushindi Mnyika na kuamuru kufungua madai kulipa gharama za  kesi na kutupilia mbali madai yake.

Naye Wakili wa Hawa Ng'humbi, Issa Maige alisema mashahidi wa upande wa wadaiwa wanajichanganya katika kutoa ufafanuzi wa kompyuta zipi zilitumika kuhesabia kura na kwamba ziliingia saa ngapi katika chumba cha kufanyia majumuisho.

Alisema msimamizi wa uchaguzi alitakiwa kutangaza matokeo ya mshindi aliyepata kura nyingi kutokana na kura halisi na ni matakwa ya lazima kisheria, kuwepo kwa kura halisi kunasaidia kuepusha udanganyifu.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles