Friday Apr 29, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Jenerali Mwita Kiaro afariki dunia

11th April 2012
Print
Comments
Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali Ernest Mwita Kiaro (87), amefariki dunia.

Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali Ernest Mwita Kiaro (87), amefariki dunia.

Jenerali Kiaro alifariki jana saa 3:55 asubuhi, baada ya kusumbuliwa ka maradhi ya Kansa ya Kibofu cha mkojo kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu, Sylvesta Kiaro, Jenerali Kiaro alikuwa anasumbuliwa na maradhi hayo kwa kipindi kirefu na alifariki akiwa njiani wakati wakimpeleka katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, jijini Mwanza.

Alisema kuwa mazishi yanatarajiwa kufanyika nyumbani kwa marehemu wilayani Tarime, Mkoa wa Mara. Hata hivyo, hakusema ni lini mazishi hayo yatafanyika kwa kuwa wanasubiri taarifa kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe, alipotafutwa na NIPASHE kuzungumzia taratibu za mazishi ya Jenerali Kiaro, alisema wanasubili taarifa kamili kutoka kwa familia ya marehemu ndipo watakapotangaza.

Alisema Jenerali Kiaro alizaliwa Julai 1, 1925 na alijiunga na Jeshi la King African Rifles Februari19, 1943 ambalo kwa sasa linajulikana kama JWTZ. Januari 31, 1964 marehemu alitunukiwa kamisheni ya kwanza (nyota).

Aliongeza kuwa Jenerali Kiaro alistaafu Machi 31, 1994.

Marehemu aliteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Septemba 1, 1988 baada ya kustaafu kwa Jenerali  David Musuguri.

Jenerali Musuguri alikuwa Mkuu wa Majeshi baada ya kustaafu kwa Jenerali Abdallah Twalipo ambaye mtangulizi wake alikuwa Jenerali Mirisho Sarakikya.

Wakati huo huo Rais Jakaya Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange, kufua tia kifo hicho.

Alisema Makamanda na wapiganaji wamempoteza kiongozi wao waliyekuwa naye karibu.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles