Wednesday May 4, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

NEC yasubiri hukumu ya Lema Mahakama Kuu

24th April 2012
Print
Comments
Godbless Lema (Chadema)

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), imesema haiwezi kuitisha uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Arusha Mjini kwa vile haijapata taarifa yoyote rasmi kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kuhusu uamuzi wa Mahakama hiyo wa kutengua ubunge katika jimbo hilo.

Mkurugenzi wa Nec, Julius Mallaba, alisema hayo alipozungumza na NIPASHE na kufafanua kuwa wataitisha uchaguzi mdogo na kuutangazia umma suala hilo iwapo watapata taarifa rasmi kutoka kwa Mahakama kuhusu hukumu hiyo.

“Hatuwezi kuutangazia umma kwa taarifa za vyombo vya habari. Tunasubiri taarifa kutoka kwa Mahakama,” alisema Mallaba.

Jimbo la Arusha Mjini lililokuwa likiwakilishwa na Godbless Lema (Chadema), liko wazi baada ya mahakama hiyo kutengua matokeo ya ubunge wake (Lema) yaliyotangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimboni humo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Gabriel Rwakibarila, Aprili 5, mwaka huu.

Kesi ya kupinga matokeo ya ubunge huo ilifunguliwa na makada watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakidai taratibu za maadili ya uchaguzi zilikiukwa kwa kuwa mshindi alitumia lugha za kashfa, matusi na kejeli katika mikutano ya kampeni aliyofanya jimboni humo.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles