Tuesday May 21, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Wanakijiji wagoma kuachia ardhi ya mwekezaji

29th April 2012
Print
Comments

Wakazi wa Kijiji cha Itilima, Kata ya Itilima wilayani hapa, wamesema kuwa hawako tayari kuliachia eneo lao lenye ukubwa wa zaidi ya kilomita za mraba 40 zilizo katika kijiji hicho ambalo kwa sasa limekaliwa na mwekezaji kwa ajili ya shughuli za uchimbaji wa madini.

Wakazi hao wameyasema hayo jana kwenye mkutano wao wa kijiji mara baada ya kubaini kuwepo kwa kile walichokielezea kuwa ni mfumo mbaya wa wao kutaka kunyang’anywa eneo hilo na mwekezaji ambaye wamesema kuwa hana sifa za kumiliki eneo hilo.

Wananchi hao walifikia uamuzi huo jana, kwa madai kuwa eneo hilo ndilo limekuwa tegemeo lao la kiuchumi na kwamba endapo litachukuliwa na Mwekezaji hali ya maisha kwao itazidi kuwa mbaya kiuchumi.

Akizungumza kwa niaba ya wanakijiji wenzake, Peter Mlwano (79), alisema kuwa kwa kutumia Sheria ya Ardhi Na.5 ya 1999, inayotambua kuwa ardhi ni mali ya kijiji, Julai 7, 2009 alikiomba kijiji cha Itilima kimilikishe kiasi cha ekari 250 za ardhi, na kuongeza kuwa aliweza kumilikishwa eneo hilo.

Akionyesha hati maalum ya maamuzi kwa eneo maalum, ambayo NIPASHE ina nakala yake, inaonyesha kuwa alimilikishwa eneo la ekari 250 Machi 31, mwaka 2009 na kusainiwa na aliyekuwa Mtendaji wa Kata ya Itilima siku hiyo hiyo.

“Pia niliweza kukabidhiwa kwa mujibu wa Sheria hiyo ya ardhi ya Toleo la Hatimiliki ya Kimila, ambayo moja ya masharti ya hati hiyo, ni pamoja na mimi ambaye natambulika kama muombaji, kumilikishwa eneo nililoomba bila ukomo kuanzia Machi 31 mwaka 2009, sasa leo nashangaa watu wamejitokeza kwa kisingizio cha uwekezaji, wakidai eneo hili ni la kwao, huu ni uonevu mkubwa na sisi hatuko tayari kuona eneo hili linamilikiwa na watu wengine eti kwa sababu tu lina madini ya dhahabu,” alisema.

Wakitoa ufafanuzi wa eneo hilo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Itilima, Abbas Masanja na Ally Ngoyeji, walisema mtu anayedaiwa kuwa ni Mwekezaji katika eneo hilo anayemiliki Kampuni ya uchimbaji madini ya DOSDAL RESOURCES AND MINING ITILIMA BUSILILI(TANZANIA) Pvt LTD, alikuwa hawajawahi kutoa taarifa kijijini hapo na badala yake walionekana kijijini hapo wakifanya shughuli za uchimbaji.

Leseni hiyo yenye Na. 4864/2007 na 4866/2007 ilionekana kuwa ilisainiwa na aliyekuwa Kamishina wa Madini kwa wakati huo, Mei 22 mwaka 2008 kwa muda ambao haukujulikana mara moja.

SOURCE: NIPASHE JUMAPILI
0 Comments | Be the first to comment