Monday May 20, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Mchujo wa Tuzo kwa waandishi waanza

21st February 2012
Print
Comments

Waandishi 39 wa magazeti na majarida, 10 wa televisheni, 20 wa redio na watatu wa vibonzo kati ya waandishi 772 waliopeleka kazi zao Baraza la Habari Tanzania (MCT) kushindania Tuzo ya Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) wameteuliwa kuingia kwenye ungwe ya mwisho itakayotoa washindi wa kila tuzo kwa mwaka wa 2011.

Taarifa ya uteuzi ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya EJAT 2011, Kajubi Mukajanga.

“Nafurahi kuwatangazia wateule walioteuliwa na jopo kushindania tuzo 18 na moja ya kazi ambazo zilianzishwa na baraza na ambazo waandishi walizitumia kuleta kazi zao. Kwa kulinganisha na miaka miwili ya nyuma, yaani mwaka 2009 ambapo zililetwa jumla ya kazi 304, 2010 kazi 437, katika shindano hili la 2011 zimeletwa kazi 772 hali inayoonyesha kuwa zoezi hili linaeleweka kwa waandishi na wanajitokeza kushindana,” alisema.

Kampuni ya The Guardian inayomiliki magazeti ya NIPASHE na The Guardian imetoa waandishi watano walioteuliwa kuingia kwenye hatua ya mwisho ya mchakato huo, upande wa magazeti na majarida utakaofanyika Machi 30, mwaka huu.

Waandishi hao ni pamoja na Paul Mabeja, Albano Midelo na Happy Severin toka gazeti la Nipashe, Monica Luwondo na mpiga picha Khalfan Said toka gazeti la the Guardian.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment