Friday May 24, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Maaskofu watofautiana hukumu ya Lema

7th April 2012
Print
Comments
  Lebulu alaumu dola, Laizer aunga mkono
Aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini Bw. Godbless Lema

Ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika mjini hapa jana iligeuka kama uwanja wa siasa baada maaskofu  kutofautiana kuhusu uamuzi wa mahakama kumvua ubunge Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini.

Tukio hilo la aina yake lilitokea katika viwanja vya mpira vya Sheikh Amri Abeid, ambapo ilifanyika ibada ya umoja wa madhehebu ya dini ya kikristo ya Siku ya Ijumaa Kuu.

Wa kwanza kuongea alikuwa Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Arusha, Josephat Lebulu, ambaye alivilaumu vyombo vya dola nchini, kunyang’anya haki za watu kwa kuwapiga makofi.

Akizungumza mbele ya umati mkubwa wa watu, waliokusanyika katika Ibada hiyo huku akishangiliwa na umati wa watu waliokuwa wakiruka kwa shangwe, alisema kuwa suala la uonevu ni kubwa kwa sasa nchini.

Alisema kuwa hata wakati wa Yesu alipigwa makofi, wakati akisulubiwa na alipouliza sababu za kupigwa makofi, aliendelea kupigwa, hivyo hali hiyo inazidi kushamiri nchini kwa watu mbalimbali kupokonywa haki zaoza msingi.

“Ngonja ninukuu maneno ya biblia kuna sehemu inasema Yesu alipigwa makofi, akauliza sababu za kupigwa kwake, hapa nafananisha na leowatu wanapigwa makofi na mahakama zetu, serikali na vyama vyao, jamboambalo linapaswa kukemewa lisiendelee,” alisema.

Alisema Askofu Lebulu, kuwa kwa sasa serikali  inatumia fedha nyingi,kuwapiga makofi wanyonge, jambo ambalo ni hatari kwa Taifa.

Aidha alimwomba Mungu kumsaidia ili asiropoke, kwa sababu katika miaka35 ya utumishi wake, hajawahi kuropoka na anamwomba Mungu amsaidie.

Mara alipomaliza kutoa hutuba hiyo kama Msemaji Mkuu, katika Umoja huo,alishangiliwa na umati wa watu, huku wakipiga vigelegele na baadhi yawatu wakiruka ruka kuashiria kuunga mkono hotuba yake

Kwa upande wake, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Dayosisiya Kaskazini na Kati, Thomas Laizer, alisimama na kuunga mkono maamuzi yaMahakama yaliyotolewa dhidi ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na kusema ni haki na kweli.

“Mimi sijawahi kuhudhuria mikutno ya kampeni ya Lema, lakini niliwahikusikia kuwa Lema alisema katika mikutano yake, kuwa mwanamke hawezikuwa kiongozi wa Malaigwanani, kama alisema hivyo kweli na anastahilihukumu,” alisema Akofu Laizer.

Kauli hiyo ilionyesha kuwachukiza waumini waliofurika katika ibadahiyo na kuanza kuguna na kushamiri mingong’ono mingi, kuashiriahawajakubaliana naye.

“Hata kama ninayosema hamyakubali, lakini huo ndio ukweli mtupu naanastahili hukumu, nafahamu wengi hamfurahii na maamuzi ya mahakamalakini Mahakama imetoa haki, hakuna kutupa lawama kwa Kikwete walaRidiwani Kikwete,” alisisitiza Askofu Laizer, huku watu wakiguna.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Raymond Mushi, alipokaribishwakusalimia waumini, alisema kuwa lazima watu wafike mahali wafahamu,haki inastahili kutolewa kwa watu kuheshimu haki na kufahamu wajibuwao.

Alisema kuwa ni wajibu wa kila mtu kupata haki, ila haki hiyo itapatikana tu kwa mtu kuheshimu wajibu wake serikalini nafamilia, kisha unaweza kudai haki kwa wengine.

uala hilo limekuja baada ya siku moja kuvuliwa ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema, ambapo wakazi wengi wa Arusha, wameonekana kuchukizwa na uamuzi wa mahakama, huku wakidai watapiga kura za hasira hata Chadema ikisimamisha jiwe watalipigia kura ili mradi
siyo CCM.


SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment