Monday Feb 8, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Mawaziri sita mikononi mwa Takukuru

7th May 2012
Print
Comments
  Wachunguzwa kuhusiana na ubadhirifu
  Kazi yapamba moto, DPP kuhusishwa
Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk. Edward Hoseah

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imeanza kufanya uchunguzi kwa kuwahoji na kufuatilia uhalali wa mali za baadhi mawaziri wote waliotajwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kuwa wanahusika kwenye ubadhirifu wa fedha za umma.

Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu jana jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Taasisi hiyo
Dk. Edward Hoseah, alisema tayari Takukuru imekwsha kuanza kuwachunguza mawaziri hao na kuanza kufuatilia uhalali wa mali zao, baada ya hapo itapeleka ripoti kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) kwa hatua zaidi za kisheria.

Alisema Takukuru haitaishia tu kuwahoji na kuwachunguza mawaziri bali itakwenda mbali zaidi kwa kuwahoji hata watendaji waliotajwa kwa ubadhirifu katika ripoti ya CAG iliyojadiliwa na Bunge mwezi uliopita.

“Taasisi yangu ni kweli imeshaanza kuwachunguza baadhi ya mawaziri wanaotuhumiwa kwa ubadhifu wa fedha za umma na wale wote waliotajwa kwenye ripoti ya CAG kwa kuwachunguza na kufuatilia uhalali wa mali zao baada ya hapo tutapeleka ripoti kwa DPP kwa hatua zaidi,” alisema Dk. Hoseah.

Ripoti ya kamati za kudumu za Bunge za Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) inayoongozwa na Zitto Kabwe, Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), inayoongozwa na Augustine Mrema na ile ya Hesabu za Serikali (PAC), inayoongozwa na John Vheyo pamoja na ya Ardhi, Maliasili na Mazingira inayoongozwa na James Lembeli, zilizua mjadala mkubwa bungeni na kutajwa kwa baadhi ya mawaziri kuwa wabadhirifu.

Ripoti hizo zilihusu ripoti ya CAG ya mwaka wa fedha wa 2009/10 ambayo ilionyesha udhaifu mkubwa wa watendaji serikalini katika kusimamia na kudhibiti fedha za walipa kodi.

Miongoni mwa waliotajwa ni pamoja aliyekuwa Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo. Anadaiwa kuhusika katika ubadhirifu wa Shirika Hodhi la Mali za Mashirika ya Umma (CHC). Alitajwa kuwa amepoteza uaminifu na uadilifu kiasi cha kusema uongo bungeni ili kuficha maslahi binafsi katika ofisi za umma.

Pia aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Cyril Chami, alitajwa kuhusika katika kumkingia kifua Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango la Taifa (TBS), Charles Ekelege, kutokana na kusema uongo katika kazi ya ukaguzi wa magari nje ya nchi.

Ekelege anadaiwa kusema uongo kuwa kuna kampuni zimepewa kazi ya kukagua magari yanayokuja nchini nje ya nchi, ambayo yanalipwa kiasi cha dola za Marekani milioni 37 (takribani Sh. bilioni 60), lakini kamati ya wabunge iliyokwenda nchi za Singapore na Hong Kong, hawakukuta kampuni hizo.

Aliyekuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda, naye anadaiwa kushindwa kusimamia matumizi bora ya fedha za umma kiasi cha kuruhusu nyumba yake kukarabatiwa kwa mamilioni ya fedha.

Wizara nyingine zilizotajwa kufuja mali za umma ni Tamisemi ambayo ilishindwa kusimamia fedha katika halmashauri mbalimbali nchini ambako ufisadi wa kiwango kikubwa umegundulika.
Aliyekuwa amebanwa na wabunge ni kuhusu ubadhirifu wa Tamisemi ni George Mkuchika, lakini amenusurika na amehamishiwa Ofisi ya Rais, Utawala Bora. Hata hivyo wakati ubadhirifu huo unafanyika mwaka wa fedha wa 2009/10 Mkuchika alikuwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Pia yupo aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, anayetuhumiwa kwa kushindwa kusimamia sekta ya madini na umeme, kuweko kwa manunuzi makubwa ya mafuta ya kuendesha mitambo ya IPTL ambayo yameongezwa bei.

Vilevile yumo aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, ambaye anatuhumiwa kushindwa kudhibiti ubadhirifu katika wizara yake kama ulivyobainika katika ugawaji wa vitalu vya uwindaji wa kitalii na usafirishaji wa wanyama hai nje ya nchi.

Aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu, anatuhumiwa kuingilia mchakato wa kumpata mzabuni wa kujenga gati namba 12 na 13 katika Bandari ya Dar es Salaam; Profesa Jumanne Maghembe aliyekuwa, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, aliyehamishiwa Wizara ya Maji anadaiwa kushindwa kudhibiti ununuzi wa pembejeo na ulipaji wa fedha za mdororo wa uchumi.

Rais Kikwete alipofanya mabadiliko ya baraza la mawaziri wiki iliyopita aliwaacha mawaziri sita ambao ni  Maige, Ngeleja, Mkulo, Mponda, Nundu, Chami na aliyekuwa Naibu Waziri wa Uchukuzi, Athuman Mfutakamba.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment