Sunday Feb 14, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Mashindano gofu wanawake yadhaminiwa NBC

23rd February 2012
Print
Comments

Kitengo cha gofu ya wanawake cha klabu ya Gymkhana kimepata udhamini baada ya benki ya Taifa ya Biashara (NBC) jana kukabidhi hundi ya Sh. milioni 21.4 kwa ajili ya kusaidia kufanyika kwa mashindano ya mchezo huo.

Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika Jumapili hii na madhumuni yake ni kupatikana kwa wa nahodha wa timu ya gofu kwa wanawake atakayewajibika kuiongoza kwenye mafanikio timu ya mchezo huo kwa kipindi kijacho.

Akizungumza katika tukio hilo, Meneja Udhamini na Matukio wa NBC, Rachel Remona Kimambo alisema: “Sisi kama NBC tunafahamu umuhimu wa michezo kwa binadamu na ndio maana tumekuwa mstari wa mbele kusaidia michezo.

“Tunafahamu umuhimu wa michezo katika kujenga afya bora ndio maana tukaamua kuungana na wanamichezo wa gofu hususani upande wa wanawake, na kuhakikisha tunasaidia mchezo huu ili uzidi kupaa.”

Gofu ni moja ya michezo maarufu katika maeneo mengi nchini ambapo mbali na burudani, imewaleta pamoja watu mbalimbali na kujenga ushirikiano, na pia kuboresha afya za wanamichezo.

"Ni matumaini yetu msaada huu utasaidia kuleta msukumo mpya katika maendeleo ya mchezo wa gofu la wanawake nchini,” alisema Rachel.

Timu ya gofu ya wanawake imekuwa na mafanikio makubwa hasa walipobakiza ubingwa nchini katika mashindano ya gofu ya wanawake yaliyofanyika mwaka jana na kuhusisha nchi mbalimbali za karibu.

Kwa kutambua umuhimu wa michezo, mwaka jana benki ya NBC iliidhamini timu ya taifa ya paralimpiki iliyokwenda kushiriki michuano ya kimataifa ya All Africa Games huko Maputo, Msumbiji.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo Nahodha wa Kitengo cha Gofu ya Wanawake, Vivienne Mwaulambo alitoa shukrani kubwa kwa NBC akisema kuwa msaada ni moja ya makubaliano ya ushirikiano na benki hiyo katika kuendeleza mchezo wa gofu hususani gofu la wanawake.

SOURCE: THE GUARDIAN
0 Comments | Be the first to comment