Wednesday May 22, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Mmoja afariki vurugu za Mtwara
Mtu mmoja amefariki dunia katika vurugu zinazoendelea Mkoani Mtwara kupinga gesi kusafirishwa, ambapo pia ofisi kadhaa na nyumba moja zimeharibiwa.

Mume, mke wagoma kuondoka mahakamani wakidai kutotendewa haki

23rd July 2012
Print
Comments
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Prof. Anna Tibaijuka,

Tafrani kubwa imeibuka katika Mahakama ya Baraza la Ardhi Mkoa wa Kilimanjaro, baada ya mahakama hiyo kutoa hukumu ya kesi namba 73/2011, ambapo wazee wawili ambao ni wadaiwa kugoma kuondoka  mahakamani hapo kwa madai kuwa hawajatendewa haki.

Wadaiwa katika kesi hiyo ni wazee Kusiriael Massawe (89) na mkewe Haikasia Massawe (79), ambao waligoma kuondoka eneo la mahakama hiyo, kwa madai mahakama imetoa upendeleo wa wazi kwa mchungaji wa kanisa la EAGT,  Elinderingo Massawe.

Kufuatia hali hiyo, Polisi walifika kwenye eneo hilo na kuwakamata wazee hao pamoja na binti yao aitwaye Beatrice Machui na kuwasweka ndani.

Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Kilimanjaro (RCO), Ramadhani akizungumza na NIPASHE, amethibitisha kushikiliwa kwa watu hao na kudai kuwa wanakabiliwa na makosa mawili ya kufanya fujo mahakamani na kusababisha usumbufu kwenye eneo hilo na kwamba upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani.

Mtoto wa Mzee Massawe, Peter Massawe, akielezea kesi hiyo, alisema awali ilifunguliwa katika Baraza la Ardhi na Nyumba Kata ya Kibosho Magharibi na baada ya kusikilizwa lilitoa ushindi kwa wazee hao baada ya kutembelea eneo hilo na kujionea ushahidi unaofanya eneo hilo kuwa mali yao.

Alisema baada ya uamuzi huo, Mchungaji Massawe, alikata rufaa katika baraza hilo ngazi ya mkoa, ambapo ilitajwa mara moja na ilivyopangiwa mara ya pili, mzee huyo alikuwa mgonjwa na kushindwa kufika mahakamani.

“Nilifuata utaratibu wa kisheria na kupata nguvu ya kisheria ya kusimamia suala hilo mahakamani, mwenendo wa kesi haukuwa wa kuridhisha, niliandika barua kwa Msajili wa Mahakama kumueleza juu ya suala hilo na jinsi ambavyo hatuna imani na Mwenyekiti wa baraza hilo, wakati ombi langu likiwa Mahakama Kuu akatumia faili jipya kutoa maamuzi” alisema.

Massawe alisema katika madai yake mahakama kuu alimshtaki Mwenyekiti huyo kuwa hawatendei haki na kumpa upendeleo wa wazi Mchungaji huyo, lakini cha kushangaza kesi iliendelea kama kawaida na kufikia uamuzi wa kutengua maamuzi ya baraza la kata.

Aidha, alimuomba Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Prof. Anna Tibaijuka, kuingilia kati na kufuatilia kwa karibu matatizo ya ardhi mkoani Kilimanjaro, kutokana na vyombo vya kutoa haki kutoa maamuzi mabovu yenye kusababisha mgogoro baina ya wananchi.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment