Wednesday May 22, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Poulsena aomba kutofananishwa na Poulsen

12th May 2012
Print
Comments
Kocha mpya wa timu ya taifa `Taifa Stars`, Kim Poulsen

Kocha mpya wa timu ya taifa 'Taifa Stars', Kim Poulsen, ameomba asifafananishwe na mwalimu anayemaliza muda wake, Jan Poulsen, kwa kuwa wao ni watu wawili tofauti.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kim alisema kuwa yeye ni tofauti na makocha wengine na kutaka kupewa ushirikiano ili kutengeneza timu nzuri ya taifa.

Alisema kuwa anajua changamoto alizonazo mbele yake baada ya kupewa na shirikisho la soka, TFF, jukumu la kuinoa Taifa Stars.

"Kwanza nataka nieleweke, pamoja na kuwa tumefanana majina na Jan, sisi ni makocha wawili tofauti," alisema na kueleza zaidi, "ninafahamu changamoto iliyopo mbele yangu lakini nipo tayari kuzishinda kwa kushirikiana na wadau wote wa mpira hapa."

Aidha, alisema kuwa amekaa nchini kwa muda wa kutosha na analielewa soka la Tanzania hivyo hatukuwa mgeni kwenye majukumu yake mapya anayoanza.

Kim ni mwalimu wa timu za taifa za vijana ambaye ametoka kuiwezesha Ngorongoro Heroes, timu ya under-23, kuitoa Sudan katika raundi ya kwanza ya michuano ya awali ya Kombe la Mataifa ya Afrika.

Alisema kuwa atakuwa akiangalia zaidi uwezo wa wachezaji kabla ya kuwaita kwenye kikosi chake.

"Kazi yangu itakuwa ikionekana uwanjani, nitakuwa nikiangalia zaidi uwezo wa wachezaji kabla ya sijamuita kwenye kikosi cha timu ya Taifa," aliongezea kusema Poulsen.

Alisema pamoja na uwezo, nidhamu nikitu ambacho kitakuwa cha kwanza kwa wachezaji wote.
Kim alisema kuwa anataandaa timu ya taifa yenye nidhamu ya hali ya juu na pamoja ushindani mkubwa.
Jana kocha huyo raia wa Denmark, alitangazwa rasmi na Rais wa Shirikisho la soka nchini (TFF), Leodgar Tenga kuwa kocha mpya wa Stars kwa mkataba wa mwaka mmoja kuchukua nafasi ya Mdenmark mwenzake huyo ambaye TFF imemtaarifu kutomuongezea mkataba mara baada mkataba wake wa sasa hivi utakapomalizika mwezi ujao.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment