Friday May 24, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Boban afurahia kuitwa Stars

16th May 2012
Print
Comments
Kiungo wa Simba, Haruna Moshi `Boban`

Kiungo wa Simba, Haruna Moshi 'Boban' ambaye amerejeshwa katika kikosi cha timu ya soka ya Tanzania (Taifa Stars) amesema kuwa amefurahishwa kuitwa tena kwenye timu hiyo na kocha mpya, Kim Poulsen.

Mbali na Boban, pia mshambuliaji wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mbwana Samatta, na mfungaji bora wa Ligi Buu Bara iliyomalizika John Bocco 'Adebayor' wa Azam, nao wamerejeshwa na kocha huyo aliyerithi mikoba ya Jan Poulsen.

Akizungumza na gazeti hili, Boban, alisema kuwa amepata taarifa hizo za kuitwa Stars lakini alikataa kueleza kama ataitikia wito huo au la.

"Nimesikia nimeitwa, nimefurahi kuitwa, nitaenda kambini," alisema mchezaji huyo kwa kifupi ambaye huwa hapendi kuzungumza na vyombo vya habari.

"Nimelala siwezi kuzungumza zaidi, nipigie baadaye," alisema Boban ambaye alirejea nchini jana saa tatu asubuhi na timu ya Simba wakitokea Sudan na kukata simu.

Baada ya kukaa benchi kwa mwaka mmoja lakini aking'aa kwenye mashindano ya Kombe la Kagame yaliyopita, mwaka jana Poulsen alimuita Boban katika kikosi cha timu ya vijana ya umri chini ya miaka 23 kilichokuwa na mechi dhidi ya Shelisheli, kiungo huyo alikacha wito huo na hivyo kuendelea kukaa nje kwenye Stars.

Hata hivyo, Poulsen aliwahi kusema kwamba Boban hana uwezo wa kucheza kwa dakika 90 jambo ambalo kocha wake wa Simba, Mserbia Milovan Cirkovic amelifanyia kazi na kiungo huyo sasa anacheza dakika zote za mchezo.

Wachezaji wa Stars walioitwa na leo wanatarajia kuanza mazoezi chini ya Kim ni pamoja na makipa; Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ally (Azam) na Deogratius Munishi (Mtibwa Sugar) wakati mabeki ni Nassor Masoud 'Chollo' (Simba), Aggrey Morris (Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Simba), Waziri Salum (Azam), Shomari Kapombe (Simba) na Juma Nyoso (Simba).

Viungo ni Mwinyi Kazimoto (Simba), Salum Abubakar (Azam), Nurdin Bakari (Yanga), Jonas Mkude (Simba), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Edward Christopher (Simba- U20), Mrisho Ngasa (Azam) na Frank Domayo (JKT Ruvu- U20).

Safu ya ushambuliaji ya timu hiyo itaongozwa na Samata, Ramadhan Singano (Simba-U20), Simon Msuva (Moro United- U20), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Boban  na John Bocco wa Azam.

Stars inayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) itaweka kambi yake katika hoteli ya Tansoma na itacheza mechi yake ya kwanza ya kirafiki chini ya Kim Mei 26 mwaka huu dhidi ya Malawi na Juni 2 itasafiri ugenini kwenda kuivaa Ivory Coast katika mechi za kusaka tiketi ya kucheza fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment