Saturday Apr 30, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Wachezaji Simba wamwagiwa mamilioni

2nd May 2012
Print
Comments
Timu ya Simba

Uongozi wa Simba jana uliwapa wachezaji wake Sh. milioni 35 ikiwa ni motisha baada ya kuifunga Al Ahly Shandy ya Sudan katika mechi yao ya kwanza ya Kombe la Shirikisho iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumapili.

Wekundu hao wa Msimbazi waliibuka na ushindi wa magoli 3-0 na sasa wako Zanzibar wakijiandaa kwa mechi yao dhidi ya Yanga itakayofanyika Jumamosi na pia ya marudiano dhidi ya Wasudan (Al Ahly).

Habari kutoka ndani ya Simba zinaeleza kwamba kiasi hicho cha fedha kilikabidhiwa kwa nahodha wa timu hiyo, Juma Kaseja ili agawane na wenzake.

Chanzo chetu kilieleza kuwa mbali na wachezaji, pia viongozi wa benchi la ufundi ambao wako chini ya Mserbia, Milovan Cirkovic walifaidika na ‘bonasi’ hiyo ya ushindi.

"Leo (jana) asubuhi tumewagawia wachezaji Sh. milioni 35 kama motisha baada ya kuwaua Al Ahly Shnady," alisema mmoja wa viongozi wa Simba.

Alisema kuwa kiasi hicho cha fedha kimetokana na kiasi cha Sh. milioni 216 kilichopatikana katika fedha za mlangoni huku nyingine zikitumika katika maandalizi ya safari yao ya kuelekea Sudan watakapokwenda kucheza mechi ya marudiano na Al Ahly.

Kiongozi huyo alisema kuwa wachezaji wa Simba wataendelea kuneemeka zaidi endapo wataifunga Yanga Jumamosi na pia watakaposonga mbele katika mashindano ya kimataifa.

Vinara hao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara wanaohitaji pointi moja ili watwae ubingwa wa ligi.

PONGEZI TFF
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa pongezi kwa Simba kutokana na ushindi mnono wa nyumbani wa mabao 3-0 dhidi ya Al Ahly katika mechi yao ya Kombe la Shirikisho.

Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, alisema kuwa ushindi huo umetokana na ushirikiano uliopo kuanzia kwa wachezaji, benchi la ufundi, viongozi, wanachama wa klabu hiyo na Watanzania kwa ujumla na hivyo wote wanastahili pongezi.

Wambura alisema kuwa wanaamini Simba haijabweteka kwa ushindi huo na badala yake wanaendelea kujiandaa vyema kwa mechi yao ya marudiano ili wafanye vizuri na kuendelea  vyema na michuano hiyo.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles