Friday May 6, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Watu 51 wafikishwa mahakamani vurugu za Ikwiriri

22nd May 2012
Print
Comments
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ernest Mangu

Watu 51 wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za ujambazi wa kuvunja, kupora mali na kufunga barabara katika vurugu zilizotokea mjini Ikwiriri, Wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani, juzi, miongoni mwao akiwamo mtoto wa miaka 12 anayetuhumiwa kwa mauaji ya mzee wa miaka 80 yaliyosababisha vurugu hizo.

Mtoto huyo, ambaye ni mchungaji wa mifugo na mkazi wa Ikwiriri (jina linahifadhiwa), anatuhumiwa kumuua mzee huyo, Seif Shamte (80), Mei 19, mwaka huu, katika Kijiji cha Nyambere, wilayani humo.

Shamte, ambaye alikuwa mkulima na mkazi wa Ikwiriri, anadaiwa kuuawa kufuatia ugomvi uliosababishwa na mtoto huyo pamoja na wenzake kulisha mifugo katika shamba lake.

Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Ernest Mangu, aliliambia NIPASHE kwa njia ya simu jana kuwa mzee huyo alifariki baada ya kuanguka alipokuwa akimkimbia mtoto huyo na wenzake waliotishia kumshambulia kwa fimbo.

“Walimtishia kwa fimbo, mzee akakimbia, lakini akaanguka na ndiyo ikawa mwisho wake hapo,” alisema Kamanda Mangu.

Mtoto huyo na watuhumiwa wenzake 50, walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Rufiji, mkoani humo jana, wakituhumiwa kutenda makosa hayo, baadhi yao kabla na wengine wakati wa vurugu hizo.

Kamanda Mangu alisema siku ya tukio, mtoto huyo alikuwa akichunga ng’ombe wa baba yake.

Alisema mtoto huyo alifikishwa mahakamani jana, lakini alisomewa mashtaka yake akiwa kwenye gari.

“Hatukumfikisha katika mahakama ya wazi. Tulimpeleka kwa gari. Tukamuomba hakimu akatoka nje, akasomewa mashtaka yake, kisha tukaomba waranti (hati) tukampeleka gerezani,” alisema Kamanda Mangu.

Kuhusu watu 50, Kamanda Mangu alisema baadhi wanatuhumiwa kwa ujambazi wa kuvamia maduka na kupora mali zilizokuwamo, wengine kuvamia mazizi ya ng’ombe, kuchinja na kugawana nyama.

Alisema wengine wanatuhumiwa kuvunja nyumba za watu na kuiba vitu vilivyokuwamo na wengine kufunga barabara na kuzuia magari kupita kwa muda mrefu.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles