Friday May 6, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

`Mfumuko wa bei tishio kwa wawekezaji`

3rd April 2012
Print
Comments

Mfumuko wa bei unaweza kuwakimbiza wawekezaji wenye nia ya kuja kuwekeza nchini iwapo utaendelea kukua kama ilivyo sasa.

Tahadhari hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa benki ya Standard Chartered, Jeremy Awori, wakati akitoa mada kwenye semina ya Mameneja wa Rasilimali Watu kutoka makampuni mbalimbali.

Semina hiyo iliyokuwa na lengo la kuangalia masuala mbalimbali ya rasilimali watu, iliandaliwa na Chama cha Wanataaluma ya Rasilimali Watu Tanzania (HRSTA).

Awori alisema tafiti zinaonyesha kuwa Tanzania ndiyo yenye mfumuko mkubwa wa bei baina ya nchi za Afrika Mashariki, jambo linaloweza kuathiri biasharana uwekezaji.

Awori alisema Tanzania ina fursa ya kukuza uchumi wake kwa kiwango kikubwa kwani imejaliwa kuwa na rasilimali nyingi kuliko nchi nyingi za Afrika.

Alisema Tanzania inamadini mengi na maliasili nyingi ambazo hazipatikani katika nchi nyingi hivyo hiyo ni fursa kubwa ya kuwezesha uchumi kupaa kwa haraka.

Awori alisema biashara baina ya Tanzania na mataifa makubwa kama China inaongezeka hivyo kuna haja kwa wanataalumahao kuichukua hiyo kama fursa kwao.

Alitoa mfano kuwa wachina wengi wanakuja kufanya miradi mikubwa katika sekta mbalimbali kama ujenzi hivyo wanahitaji huduma mbalimbali kama za kibenki.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles