Thursday May 5, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Kikwete amlilia dereva wa Ikulu

7th May 2012
Print
Comments
Rais Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma, wakitoa heshima za mwisho kwa marehemu Deokalyus Makwasinga, aliyekuwa dereva wa Ikulu kwa miaka mingi. (PICHA: IKULU)

Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma, jana waliungana na waombolezaji kuuaga mwili wa aliyekuwa mtumishi wa Ikulu, marehemu Deokalyus Makwasinga, nyumbani kwake Kimara-Kilungule, Dar es Salaam.

Taarifa ya Ikulu iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana jijini Dar es Salaam ilieleza kwamba marehemu Makwasinga, ambaye alikuwa dereva wa miaka mingi Ikulu, alifariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kufuatia ajali mbaya ya gari eneo la Kimara-Korogwe, Msikitini, Dar es Salaam usiku wa kuamkia Ijumaa iliyopita.

Mara baada ya shughuli ya kuaga, mwili wa marehemu Makwasinga, ulianza safari ya kupelekwa Mahenge mkoani Morogoro ambako atazikwa.

Marehemu ameacha mjane na watoto watatu.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles