Sunday May 1, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Nchunga:Wazee Yanga wamefanya uhuni

20th May 2012
Print
Comments
Mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga

Mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga alisema amegoma kuhudhuria mkutano wa leo ambao aliuitisha mwenyewe kutokana na wazee wa klabu hiyo kufanya uhuni.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Nchunga ambaye anasakamwa na kundi la wazee kuachia madaraka Yanga alisema mkutano baina yake na Baraza la Wazee alioitisha wiki iliyopita ulibadilishwa kihuni na kundi hilo na kuuita mkutano mkuu wa wanachama.

"Wazee wamefanya uhuni kwa sababu wamedandia mkutano wangu mimi na wao na kutangaza kuwa huo mkutano wa kesho ni mkutano mkuu wa wanachama," alisema Nchunga.

"Ni uhuni kwa sababu hatukupanga wala kukubaliana hivyo na wazee.

"Katika Kamati ya Utendaji, tulikubaliana nikutane na wazee kwa lengo la kujadili mambo yanavyokwenda pamoja na mvutano wao na uongozi.

"Sasa nimeshangazwa kuona wazee wakiita wanachama wote na kutangaza kuwa huu ndio mkutano mkuu kitu ambacho si cha kweli.

"Kwa kuona hili nimeuhairisha mkutano huu... hautofanyika kesho (leo)," alisema Nchunga.

Alisema kuwa kitu kingine kilichomshangaza ni kitendo cha wazee hao kuwatangazia wanachama kufika kwenye mkutano huo ili kumshinikiza ajiuzulu uongozi wa klabu hiyo.

"Kwa kuwatangazia wanachama mambo hayo nimeona kabisa kutatokea uvunjifu wa amani kwenye huu mkutano ambao mimi nilipanga kukutana na wazee tu," alisema.

"Kwa hiyo kwa kuliona hili nimeona nisifanye mkutano tena na huo mkutano wao mimi sitakuwepo kwa sababu siutambui."

Aidha, alisema kuwa mkutano pekee utakaojadili kujiuzulu kwake ni mkutano mkuu wa klabu hiyo unaotambulika kikatiba ambao tayari ametangaza utafanyika Julai 15.

"Mimi na uongozi mzima wa klabu hii tumeingia madarakani kwa kufuata taratibu za kikatiba," alisema.

"Kama baadhi ya wanachama wanataka tuondoke madarakani basi wasubiri kwenye mkutano mkuu lakini sio kueneza maneno ya chuki na kushinikiza vitu ambavyo havipo."

SOURCE: NIPASHE JUMAPILI
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles