Saturday Apr 30, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Yanga yapania kushindia mashabiki

22nd April 2012
Print
Comments
Beki wa kati wa Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro'

Beki wa kati wa Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro' amesema timu hiyo ambayo kimahesabu haina nafasi ya kuwa moja ya wawakilishi wawili wa nchi katika michuano ya klabu ya Afrika mwakani, itaingia uwanjani leo kwa lengo la kupata ushindi dhidi ya Polisi Dodoma bila kujali imeshapoteza pia ubingwa wa ligi kuu ya Bara.

Akizungumza na Nipashe jumapili jana 'Canavaro' wachezaji wamejipanga kuhakikisha wanashinda mchezo wa leo na wa mwisho dhidi ya Simba utakaochezwa Mei 5 kwenye Uwanja wa Taifa.

"Kweli hatupo kwenye mbio za ubingwa... lakini hii si sababu ya sisi kufungwa (kesho), tutapigana kuhakikisha tunashinda," alisema 'Canavaro' ambaye timu yake iliharibikiwa wiki hii baada ya vipigo viwili ndani ya siku nne na kutupwa kwa rufaa ya kupinga kupokonywa pointi za Coastal Union.

"Haya matokeo mengine lazima mashabiki wajue ndio mpira ulivyo."

Yanga inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 43 kutokana na michezo 23, pointi saba nyuma ya Azam iliyobakisha mechi tatu pia na ambayo mwenendo wake unaonyesha haitakosa pointi tatu katika michezo yake hiyo kuiengua Yanga kimataifa.

Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 56 lakini ikiwa mbele kwa mchezo mmoja zaidi ya Yanga na Azam.

Ligi hiyo itafikia mwisho Mei 5 mwaka huu wakati Simba na Yanga zitapoonyeshana kazi kwenye uwanja wa Taifa huku Azam ikicheza na Kagera Sugar kwenye uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Kocha Kostadian Papic leo ataiongoza Yanga kwa mara ya mwisho baada ya kutangaza kuachana na timu hiyo pindi mkataba wake utakapomalizika keshokutwa.

Alisema kuwa pamoja na kupoteza ubingwa, hawatakuwa tayari kufungwa mchezo wa leo.

SOURCE: NIPASHE JUMAPILI
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles