Monday May 20, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Zawadi zatajwa pool Taifa

16th June 2012
Print
Comments
Oscar Shelukindo


Bingwa wa fainali za taifa za mashindano ya pool yanayodhaminiwa na TBL atazawadiwa sh. milioni tano.

Meneja wa wadhamini wakuu wa mchezo huo nchini, Oscar Shelukindo aliwambia waandishi wa habari juzi jijini Dar es salaam kuwa zawadi za mwaka huu zimeboreshwa kwa asilimia 20 ikilinganishwa na zawadi za mwaka jana.

Shelukindo alisema kuwa lengo la kuboresha zawadi hizo ni katika kuhakikisha mchezo huo unazidi kukua siku hadi siku na hatimaye uwe mmoja wa michezo tishio nchini kwa kuwa na mashabiki kila kona ya Tanzania.

Alisema kuwa wakati bingwa wa taifa atajinyakulia kiasi hicho cha fedha, mshindi wa pili ataondoka na sh. milioni 2.5, mshindi wa tatu atazawadiwa sh. milioni 1.2 huku mshindi wa nne kwa upande wa timu akipewa sh.700,000.

Kwa mchezaji mmoja mmoja (wanaume), alisema Shelukindo,  bingwa wa taifa atajizolea Sh.500,000, mshindi pili Sh.250,000, mshindi wa tatu Sh.2000  na mshindi wa nne Sh.150,000.
 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment