Thursday Jun 20, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Mishahara hewa yabainika Mahakama, Bunge

23rd April 2012
Print
Comments
Mthibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, (CAG), Lodovick Utouh

Mahakama na Bunge ni miongoni mwa wizara, idara na wakala wa serikali, wanaonyeshwa katika ripoti ya Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuwa imelipa mishahara hewa yenye thamani ya Sh 142,715,827.99.

Kwa mujibu wa ripoti inayoishia mwaka wa fedha Juni 2011,  iliyotolewa na Mthibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, (CAG), Lodovick Utouh, fedha hizo zililipwa kwa watumishi waliostaafu, walishaoindoka kazini na wasio na sifa.

Alizitaja maeneo zilizozolipwa ni Mahakama Kuu na kiasi cha fedha katika mabano kuwa ni (18,018,540), mahakama za wilaya na mahakama za mwanzo (56,705,420), Bunge (11,078,420), Wizara ya Viwanda na Biashara (27,099,393.30), Wizara ya Nishati na Madini (8,177,716.16)  na Wizara ya Habari (13,040,171.27).

Aidha, alisema wizara, idara na wakala wa serikali walikuwa na matumizi ya Sh 8,076,574,791.42 hayakuwa na nyaraka. Baadhi ya maeneo yaliyotajwa katika ripoti hiyo ni Mahakama kuu, mahakama za wilaya na mwanzo, Bunge, Wizara ya Nishati na Madini, Mahakama ya Kazi, Jeshi la Kujenga Taifa, Tume ya Kupambana na Ukimwi (Tacaids) na Idara ya Uhamiaji.

Alisema, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Ofisi ya Katibu Tawala mikoa ya Dodoma, Singida, Mbeya, Morogoro, Dar es Salaam, Manyara na Arusha.

Katika ripoti hiyo inaonyesha malipo y ash 1,471,933,333 yenye mashaka katika Ofisi ya Makamu  wa Rais, ofisi za mikoa ya Tabora na Manyara. Utouh alisema malipo yenye thamani ya Sh 31,027,797,820 yamelipwa kwa wazabuni mbalimbali katika mwaka huu wa fedha.

Katika ukaguzi uliofanywa katika wizara, idara, wakala na ofisi za makatibu tawala imeonyersha kuwa bidhaa zenye thamani ya fedha hizo zililipiwa lakini hazikupokelewa. 

Alizitaja Wizara ya Maji (132,598,919), Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (30,865,918,901), Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi (9,000.000), Ofisi ya katibu Tawala Singida (19,000,000) na Ofisi ya Katibu Tawala Manyara (1,280,000).

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment