Wednesday May 4, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Biashara ya madini sasa kufanyika hapa nchini

27th April 2012
Print
Comments
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja

Wafanyabiashara wakubwa wa madini na vito wameafiki mpango wa serikali kununua bidhaa hizo ndani ya nchi badala ya kununua kwa njia ya panya baada ya serikali kupata hati ya uasilia ya madini na vito.

Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alisema hayo wakati akifungua maonyesho ya kimataifa ya madini na vito yanayoendelea jijini hapa.

Maonyesho hayo yamewaleta wafanyabishara wakubwa zaidi ya 100 wa madini na vito kutoka Marekani, India, Ulaya na Afrika Kusini.

Alisema hatua ya wafanyabiashara hao kukubali kununua madini na vito moja kwa moja hapa nchini, itaiwezesha serikali kupata mapato makubwa zaidi, wazawa kupata ajira na hivyo kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla kwa kuwa yatakuwa yanaongezwa thamani hapa hapa nchini.

Alisema hatua hiyo pia itazuia wafanyabiashara wanaotumia njia za panya kununua madini na vito washindwe kwa kuyauza kwa sababu hayatakubaliwa katika masomo ya dunia kwa vile hayatakuwa na hati asilia.

Pia alisema itasaidia kudhibiti biashara ya fedha haramu ambazo zinafadhili ugaidi na mapigano ya nchi kwa nchi au wenyewe kwa wenyewe.

“Maonyesho haya ni fursa kwa sisi kuwafikishia ujumbe wanunuzi wakubwa hapa Tanzania kuwa tumepata cheti cha uhalisia wa madini na vito...wamekubali kutuunga mkono, na wamesema kuwa hawatanunua madini na vito kwa njia za panya, isipokuwa watakuja moja kwa moja kununua hapa,” alisema.

Alisema dhamira hiyo ya serikali imepokelewa vizuri na wamepata nafasi ya kutangaza vito na madini yaliyopo nchini.

Alisema maonyesho hayo yalikuwa yakifanyika miaka ya 90 lakini yalisimama kwa muda na kwa sasa serikali imeamua kuyafufua na kwamba yatakuwa yakifanyika kila mwaka.SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles