Saturday May 25, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Mintanga mahakamani tena Juni 11

23rd May 2012
Print
Comments
Rais wa zamani wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (TBF), Alhaji Shabani Mintanga

Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Dar es Salaam itaendelea kusikiliza ushahidi wa upande wa Jamhuri wa kesi ya kula njama na kusafirisha dawa za kulevya kilo 4.8 inayomkabili Rais wa zamani wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (TBF), Alhaji Shabani Mintanga Juni 11, mwaka huu.

Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa mbele ya Jaji Dk. Fauz Twaib wa mahakama hiyo.

Awali, mahakama hiyo ilisikiliza ushahidi wa mashahidi watatu wa Jamhuri ambao ni Godfrey Mroso ambaye ni mfanyakazi wa Kampuni ya Anvelope Travel Agency aliyedai kuwa yeye ndiye alitengeneza tiketi tatu ambazo aliomba zipokelewe na mahakama kama vielelezo, ombi ambalo lilipingwa vikali na mawakili wa utetezi, Jerome Msemwa na Yassin Member, kwa madai kuwa tiketi hizo ni nakala badala kuwasilisha tiketi halisi.

Mahakama ilitupilia mbali maombi hayo ya kupokea nakala za tiketi ambapo upande wa Jamhuri, Wakili Mwandamizi wa serikali Prudence Rweyongeza alimleta shahidi wa nne.

Shahidi huyo ni Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Charles Ulaya lakini kutokana na ushahidi ulitolewa wakati shahidi wa tatu anataka kutoa vielelezo hivyo vitatu vilionekana vinalingana na vya shahidi wa nne ambavyo vimetengenezwa kwa teknolojia ya kielektroniki ni nakala siyo halisi.

Mintanga alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mwaka 2008 akikabiliwa na kesi hiyo ambapo kutokana na mashtaka yanayomkabili kutokuwa na dhamana kisheria yuko mahabusu hadi kesi yake itakapotolewa uamuzi.


SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment