Thursday May 23, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Vikongwe wazua tafrani mahakamani

21st July 2012
Print
Comments
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka

Tafrani imeibuka katika Mahakama ya Baraza la Ardhi mkoa wa Kilimanjaro, baada ya mahakama hiyo kutoa hukumu kwa wazee wawili ambao waligoma kuondoka mahakamani hapo kwa madai kuwa hawajatendewa haki.

Wadaiwa katika kesi hiyo ni Kusiriael Massawe (89) na mkewe Haikasia Massawe (79), ambao waligoma kuondoka eneo la mahakama hiyo, kwa madai kuwa mahakama hiyo imetoa upendeleo wa wazi kwa mchungaji wa kanisa la EAGT,  Elinderingo Massawe.

Kufuatia hali hiyo, Polisi walifika kwenye eneo hilo na kuwakamata wazee hao pamoja na binti yao  Beatrice Machui, na kuwasweka ndani.

Mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Kilimanjaro (RCO), Ramadhani akiongea na NIPASHE, amethibitisha kushikiliwa kwa watu hao na kudai kuwa

wanakabiliwa na makosa mawili ya kufanya fujo mahakamani na kusababisha usumbufu kwenye eneo hilo na kwamba upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani.

Mtoto wa Mzee Massawe, Peter Massawe, akielezea kesi hiyo alisema awali ilifunguliwa katika baraza la ardhi na nyumba kata ya Kibosho Magharibi na baada ya kusikilizwa ilitoa ushindi kwa wazee hao, baada ya kutembelea eneo hilo na kujionea ushahidi unaofanya eneo hilo kuwa mali yao.

Alisema baada ya uamuzi huo, Mchungaji Massawe, alikata rufaa katika baraza hilo ngazi ya mkoa, ambapo ilitajwa mara moja na ilivyopangiwa mara ya pili, mzee huyo alikuwa mgonjwa na kushindwa kufika mahakamani.

Massawe alisema katika madai yake mahakama kuu alimshtaki Mwenyekiti huyo kuwa hawatendei haki na kumpa upendeleo wa wazi Mchungaji huo, lakini cha kushangaza kesi iliendelea kama kawaida na kufikia uamuzi wa kutengua maamuzi ya baraza la kata.

Aidha, alimuomba Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, kuingilia kati na kufuatilia kwa karibu matatizo ya ardhi mkoani Kilimanjaro, kutokana na vyombo vya kutoa haki kutoa maamuzi mabovu yenye kusababisha mgogoro baina ya wananchi.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment