Monday May 2, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Kampuni zaburuzana Ewura

10th April 2012
Print
Comments
Ewura

Kampuni kadhaa za uuzaji mafuta nchini zimeshtukiana na kuamua kufikishana kwa mamlaka za usimamizi kutokana na kukithiri kwa vitendo vya uchakachuaji wa mafuta ya petroli na dizeli.

Kampuni hizo ni Gapco, Engen, Mogas, Tiper, Natoil, Hass, Kobil, Oil Com na Puma Energy ambayo zamani ilikuwa ikijulikana kama BP Tanzania.

Kukithiri kwa uchakachuaji huo wa mafuta kumesababisha baadhi ya shehena zilizokuwa zikisafirishwa kwenda nchi jirani kukataliwa.

Aidha, Chama cha Wafanyabiashara wa Mafuta nchini (Taomac), kimelazimika kuandika barua kwenda kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) ili kuingilia kati suala hilo.

Barua ya Taomac ya Aprili 5, mwaka huu, kwenda Ewura, ilisema wafanyabiashara wa mafuta wanahisi kuwa mafuta yaliyoingizwa nchini yamechakachuliwa kwa kuchanganywa na ethanol.

Katika barua hiyo, Taomac pia imeomba Ewura kuichunguza kampuni moja ya kigeni kama ina nyaraka muhimu ya ubora wa bidhaa zikiwa kwenye meli na bandarini kwa shehena ya mafuta ya miezi mitatu ya nyuma.

Barua hiyo ya Taomac iliyosainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wake, Salum Bisarara, iliongeza kwamba kwa kuwa suala hilo ni la kibiashara, Ewura ifanye jitihada za kupata majibu kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kuhusiana na sampuli za mafuta zilizopelekwa kwake.

Nakala ya barua ya Taomac, pia imetumwa kwa Wizara ya Nishati na Madini, Mwenyekiti wa Kamati ya Kuratibu Uagizaji wa pamoja na kwa Mkurugenzi wake Mkuu.

Kwa upande wa uuzaji wa mafuta katika nchi jirani, tayari Rwanda imekataa kupokea shehena ya mafuta ya kampuni ya Mogas kwa madai yamechakachuliwa.

Shehena nyingine ya mafuta ya Kampuni ya Mogas inashikiliwa mjini Lubumbashi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) kusubiri matokeo ya uchunguzi.

Mbali ya Mogas, kampuni ya Hass nayo ilisema malori yake manne yanashikiliwa mjini Kigali, Rwanda na yamezuiwa kupakua mafuta.

Kwa upande wake, Kampuni ya Oil Com ilisema malori yake 10 yalikataliwa na wateja kupakua mafuta na tayari wateja katika vituo vyake vilivyoshusha mafuta hayo wameanza kulalamika.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles