Friday May 6, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Moto wa CAG kuwababua watendaji Sengerema

10th May 2012
Print
Comments
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo, amewaagiza watumishi wote waliotuhumiwa kufuja fedha za halmashauri waandikiwe barua kujibu tuhuma zinazowakabili ndani ya siku 14.
 
Hatua hiyo imetokana na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)  kubaini ubadhirifu mkubwa wa fedha za halmashauri hiyo ambapo zaidi ya Sh. bilioni mbili kutumika kutumika kinyume cha maelekezo ya serikali huku baadhi yao wakishindwa kusimamia idara zao.

Idara zilizobainika kuwa na ubadhirifu wa fedha hizo zilizotolewa na serikali kwa ajili ya miradi ya maendeleo ni Idara ya Manunuzi, Fedha, Maji, Kilimo, Ardhi, Ujenzi na Bodi ya Zabuni na baadhi ya watumishi waliofanya tathmini ya miradi ya maendeleo ikiwemo ya barabara.
 
Ndikilo alisema watendaji 21 wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema wanadaiwa kujihusisha na ubadhirifu wa mamilioni ya fedha za miradi ya maendeleo na kwamba siku zao zinahesabika baada ya kuwapa siku 14 kutoa utetezi wao.
 
Aliwataka madiwani kutumia mwanya huo kuisafisha halmashauri yao kutokana na kukithiri kwa ubadhirifu wa fedha na kuwafananisha watumishi waliohusika katika upotevu wa fedha hizo na mdudu ajulikanaye kwa jina la dumuzi.
 
‘’Haya ni maagizo yanayotokana na ripoti ya CAG baada ya kubaini upotevu mkubwa wa fedha za serikali…tumeamua kuanza kuchukua hatua,na nimewaagiza madiwani watumie muda huu kuisafisha halmashauri yao, baada ya kulalamika kwa muda mrefu juu ya uwepo wa dumuzi, lakini nimewatahadharisha wasitoe maamuzi ya kuonea au kupendelea mtu, bali haki itendeke,’’ alisema Ndikilo.
 
Fedha zilizotumika vibaya ni ukiukwaji wa manunuzi Sh. milioni 733.9, usimamizi dhaifu na matumizi mabovu ni Sh. milioni.749.3, ukiukwaji wa malipo Sh. bilioni 1.4, hali iliyopelekea halmashauri hiyo kupata hati yenye mashaka mwaka 2009/10 na 2010/11.
 
Alisema watuhumiwa hao wanatakiwa kuwasilisha utetezi wao wa maandishi kwenye kikao cha baraza la madiwani ambao watawajadili na kutoa maamuzi isipokuwa wakuu wa idara ambao atawaundia tume maalum isiyozidi watu wane kwa ajili ya kupitia utetezi wao iwapo utakuwa unakidhi haja ya ripoti ya CAG au la.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles