Thursday Jun 20, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Bajeti ndogo mwaka huu

9th June 2012
Print
Comments

Wizara ya Fedha imesema kitendo cha wafadhili kutoa fedha kidogo tofauti na walivyoahidi katika bajeti kuu ya mwaka jana, kumeifanya wizara hiyo kushindwa kugawa fedha kwa kadri zilivyoidhinishwa na Bunge.

Hayo yalisemwa na Mhasibu wa Idara ya Uhasibu katika wizara hiyo, Batuli Killo,  alipokuwa akizungumza katika Kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali Kuu (PAC), mjini hapa.

“Bajeti yetu imekuwa ikitegemea wafadhili, wanaahidi lakini wanaleta kidogo, wizara tunashindwa kutoa fedha kulingana zilivyoidhinishwa,” alisema Killo.

Alisema hali hiyo inafanya kutegemea makusanyo yanayotokana na vyanzo vya mapato vya ndani.

Hata hivyo, alisema makusanyo ya fedha kutoka vyanzo vya ndani yameshindwa kutosheleza mahitaji.

Killo alilazimika kutoa ufafanuzi huo, baada ya Kamati hiyo katika kikao kilichokuwa kikiongozwa na Mbunge wa Kibiti (CCM), Abdul Marombwa, kumtaka kufanya hivyo, baada ya kusikiliza changamoto zinazoukabili  mkoa wa Dodoma.

Mbunge wa Chilonwa, Ezeckiah Chibulunje, ndiye aliyemtaka mhasibu huyo kutoa maelezo kutokana na changamoto alizosikia kutoka Sektarieti ya Mkoa wa Dodoma.

Awali Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Rehema Madenge, alisema mkoa unakabiliwa na changamoto ya kushindwa kukamilisha jengo la jipya la mkuu wa mkoa na jengo uzazi kwa muda uliopangwa kutokana na kutopewa kiasi cha fedha kilichoidhinishwa na Bunge.

Alisema jengo hilo ambalo linajengwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma , litakuwa na uwezo wa kuhudumia wanawake 180.

Alisema kutokana na ufinyu wa nafasi katika wodi ya wanawake waliojifungua inawalazimu kulala watatu ama wawili kila kitanda.

“Hivi sasa imebakia shilingi milioni 800 kukamilika kwa jengo hilo lakini hali inavyoonekana huenda fedha hizo zikaongezeka,” alisema.

Alisema hata fedha wanazozipata kutoka Hazina kwa ajili ya kuhudumia hospitali hiyo kwa asilimia kubwa zimekuwa zikitumika kulipia madeni.

Alitoa mfano huduma za usafi, ulinzi na chakula ambazo zimebinafsishwa, jambo ambalo limewafanya  kushindwa kulipia na hivyo kujikuta wakiendelea kuzalisha madeni.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment