Wednesday May 4, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Mradi wa kukomesha maadili potofu ya walimu wazinduliwa

12th May 2012
Print
Comments

Mradi wa jifunze bila Woga unaolenga  kukomesha vitendo vya ukatili mashuleni utakaoshirikisha wanafunzi zaidi ya 56,000 kutoka shule 53 za sekondari na msingi na walimu 768 umezinduliwa rasmi. 

Masanduku maalumu kwa wanafunzi ili kukusanya kura zao za maoni dhidi ya walimu wanaokiuka maadili ikiwemo vitendo vya kufanya mapenzi na wanafunzi, na ukiukaji maadili ambapo walimu wengi wamedai unatishia kibarua chao.

Akizundua mradi huo rasmi juzi kwa kufungua masanduku yatakayotumika  na kuhuduhuriwa na wanafunzi ziadi ya 3000 kutoka shule za Geita na Mseto mjini hapa. Katibu Tawala Wilaya ya Geita Bwana Moses Minga alisema umefungua ukurasa mpya katika kukomesha vitendo vya ukatili mashuleni, ingawa alitahadharisha kutotumiwa fursa hiyo kukomoa walimu kutokana na pia kuwepo kwa baadhi ya wanafunzi wakaidi mashuleni.

Aliongeza kuwa serkali inauthamini mchango unaotolewa na mashirika ya hiari likiwemo la Plan International Wilayani Geita linalofadhiri mradi huo wa Jifunze Bila Woga utakaowanufaisha  zaidi ya wanafunzi 56,000 katika shule 53 zikiwemo za sekondari kumi na msingi 43 ambapo pia walimu zaidi ya 760 watakuwemo katika mradi huo.

Awali wakati wa uzinduzi wa mradi huo, Meneja wa Plan Wilaya ya Geita Bwana Daniel Kalimbiya alisema mradi huo utekelezaji wake utafuatiliwa na kuratibiwa na wadau kutoka sekta za Mahakama, Polisi, Elimu, Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Habari na Watendaji wa vijiji na Kata kupitia mtandao uliozinduliwa mwezi uliopita baada ya semina ya siku tatu iliyowashiriksha wadau kutoka sekta hizo.

Bwana Kalimbiya aliongeza kuwa mradi huo umezinduliwa kutokana na matokeo ya utafiti uliofanywa na mashirika na Taasisi tofauati ndani na nje ya nchi kubaini kuwa zaidi ya asilimia 70 ya wanafunzi wanaokatisha au kukimbia shule katika shule za Msingi na Sekondari hutokana na vitendo vya ukatili mashuleni unaoafanywa na walimu kwa wanafunzi ikiwemo kutakiwa mapenzi kwa wanafunzi na walimu wao  na wanapokataa huibuka uadui mkubwa.

Aliongeza kuwa katika mradi huo zoezi la upigaji kura za maoni pia litawahusisha wanafunzi wakike na wakiume wanaokuwa kero kutokana na kuwatendea ukatili wanafunzi wenzao kama vile kuwalazmisha kushiriki migomo isyo na tija na fujo wakati wa masomo hivyo nao watahusihwa katika zoezi hilo litakalokuwa endelevu. Pia walimu wa kike wanaowataka wavulana kimapenzi nao watatajwa katika zoei hilo na wale wanaoadhibu bila kuzingatia taratibu nao watakuwemo.

Baadhi ya wanafunzi waliohojiwa wamedai kuwa mradi huo unaweza kuwa mkombozi mkubwa kwao iwapo utetekelzwa kama ulivyokusudiwa wakati kwa upande wao walimu wengi wao wameonekana kupatwa na hofu juu matokeo ya utekelezaji wake wakihofia kuweka mchanga katika kitumbua chao kutokana na kuwepo kwa ukikukwaji mkubwa wa maadili kwa walimu na wanafunzi wenyewe hasa katika vitendo vya ngono.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles