Tuesday May 21, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Ngorongoro Heroes hoi tena

17th July 2012
Print
Comments
Kocha mpya wa timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) Jakob Michelsen

Kocha mpya wa timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) Jakob Michelsen ameendelea na mwanzo mbaya wa ajira yake baada ya jana kukumbana na kipigo cha pili mfululizo wakati timu yake ilipolala 2-1 dhidi ya Rwanda katika mechi yao ya kimataifa ya kirafiki kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika mechi ya kwanza baina ya timu hizo iliyochezwa Jumamosi kwenye uwanja wa Chamazi unaomilikiwa na klabu ya Azam, Ngorongoro Heroes ilala kwa 2-0 dhidi ya vijana hao kutoka kwa Rais Paul Kagame.

Mechi hizo ni sehemu ya maandilizi ya Ngorongoro Heroes kujiweka sawa kabla ya kuikabili Nigeria katika mechi za mchujo wa michuano ya Mataifa ya Afrika kwa vijana 2013.

Magoli yote ya Rwanda yalifungwa na Nshimiyimana Emran katika dakika ya 2 na 53 na goli pekee kwa Ngorongoro Heroes lilifungwa na Atupele Green kwa penalti katika dakika ya 30 baada ya Ramadhani Singano ‘Messi’ kukwatuliwa na Bayisenge Emery ndani ya eneo la penalti.

Ngorongoro Heroes ambayo katika raundi ya kwanza ya michuano hiyo iliitoa Sudan, itacheza mechi ya kwanza ya raundi ya pili Julai 29 mwaka huu dhidi ya Nigeria kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Rwanda wanatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Nigeria Julai 24 jijini Kigali, Rwanda kabla Nigeria haijaivaa Ngorongoro Heroes.
 

 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment