Sunday May 1, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Vua gamba vaa gwanda kutingisha kusini

11th May 2012
Print
Comments
Katibu wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza kuandaa awamu mpya ya operesheni zake, ambayo safari hii kimesema kitapeleka nguvu zake katika mikoa ya Kanda ya Kusini, kuanzia Lindi na Mtwara, ili kuuhamasisha umma kuleta mabadiliko na uwajibikaji serikalini.

Katibu wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika, alisema jana kuwa ratiba rasmi ya lini operesheni hiyo itaanza, kiongozi wa chama atakayeiongoza na siku ambazo itafanyika, itatolewa baadaye.

Alisema operesheni hiyo imelenga kushughulikia mambo matatu; la kwanza likiwa ni kusimamia uwajibikaji katika ngazi zote za serikali, ili kuhakikisha changamoto zote zinazolikabili taifa zinashughulikiwa.

Mnyika, alisema jambo la pili litakaloshughulikiwa na operesheni hiyo, ni kutoa elimu ya kisiasa kwa umma kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na la tatu, ni kujenga organaizesheni ya chama mijini na vijijini.

Alisema mamuzi ya kupelekwa nguvu za operesheni hiyo katika mikoa ya Kanda ya Kusini yalifikiwa na Kamati Kuu (CC) ya Chadema.

Mnyika alisema awali CC ilipanga operesheni hiyo kufanyika mwanzoni mwaka huu, lakini ikashindikana kwa vile kipindi hicho kilikuwa ni cha majira ya mvua katika mikoa hiyo.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles