


Umoja wa Ulaya EU umetoa Euro milioni 2.5 (Sh. bilioni tano) kwaTanzania, kusaidia miradi ya maendeleo kwa lengo la kutoa fursa za ajira na kukuza uchumi.
Naibu Ofisa Mhidhinishaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Ulaya kutoka Wizara ya Fedha, Samwel Marwa, alisema tayari mkataba wa fedha hizo ulishasainiwa wanachosubiri ni wadau mbalimbali kuandika michanganuo ya miradi yao.