Friday May 6, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

M24.7/- za Papic zaibadili Yanga

28th April 2012
Print
Comments

Uongozi wa klabu ya Yanga ambao unadaiwa sh. milioni 24.75 za mshahara wa miezi mitatu wa kocha wake Kostadian Papic umebadili mawazo ya kumtema na kusema pande hizo zitakaa keshokutwa kutafuta ufumbuzi.

Papic alimaliza mkataba wa miezi sita na Yanga Jumanne na klabu hiyo haikuwa na nia ya kuendelea naye hivyo kumfanya kocha huyo kuapa kuwa ataifikisha timu hiyo katika vyombo vya kimataifa kudai haki yake. 

Akizungumza na NIPASHE jana, Katibu Mkuu wa Yanga Selestine Mwesigwa alisema watakutana na kocha huyo keshokutwa kujadiliana.

"Siwezi kuzungumza kwa undani sana lakini kwa sasa tumeanza mazungumzo na kocha (Papic) kuangalia nini tufanye," alisema.

"Sisi hatuna ugomvi naye, yeye ni kocha wetu tutakaa naye kuangalia tunafanya nini kwenye mkataba wake."
Alipoulizwa juu ya taarifa hizo za uongozi wa Yanga kuwa na mazungumzo naye keshokutwa, Papic alisema hakuna jambo lolote aliloambiwa na kusisitiza kuwa anachotaka ni kulipwa kwa mshahara wa miezi mitatu.
Papic alisema anaidai klabu hiyo zaidi ya dola za Marekani 15,000 (sh. milioni 24.75).

Hata hivyo alisema kuwa yuko tayari kukutana na uongozi wa klabu hiyo na kuwasikiliza kile watakachomwambia.

Kwa mujibu wa Mwesigwa, Papic anamaliza mkataba wake mwisho mwa msimu huu wa ligi kuu ya Bara na kusisitiza kuwa mkataba unaweza kuongezeka.

Akizungumzia kiasi cha madai ya mshahara wa kocha huyo, Mwesigwa alisema kuwa suala la mshahara wa kocha huyo ni siri kati ya klabu na kocha na hawapo tayari kuliweka wazi.

Hata hivyo alisema kuwa ni kweli Papic anadai mshahara ambao umechelewa na kusisitiza kuwa suala hilo ni siri ya klabu na mwalimu.

Yanga inahaka kumlainisha Papic aendelee kuifundisha licha ya mkataba wake kumalizika, na licha ya kuwa deni kubwa la mshahara wake kutokana na kuwepo kwa mchezo dhidi ya watani wa jadi Simba Mei 5.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles