Wednesday May 4, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Mbunge wa Arumeru Mashariki asakwa na polisi

8th May 2012
Print
Comments
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema)

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema), pamoja na wenzake watatu wanasakwa na polisi kuhusiana na kauli ambazo polisi wanadai kuwa ni za uchochezi/uhaini ambazo zilitolewa kwenye mkutano wa hadhara wa ‘Vua gamba, Vaa gwanda.’

Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi nchini, DCP Isaya Mngulu, alisema mkutano huo ulifanyika katika viwanja vya NMC Unga Ltd jijini hapa Jumamosi iliyopita.

“Tunamtaka aje hapa polisi kuhojiwa kwa maneno yaliyotamkwa kwenye mkutano wa Chadema Jumamosi iliyopita ambay o mengine yanamhusu,” alisema wakati akizungumza na wanahabari ofisini kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa.

Alisema wamekuwa wakimpigia simu za kumtaka kwenda polisi kuhojiwa tangu Jumamosi, lakini mara zote simu zake zinaonyesha kuwa zimezimwa.

Hata hivyo, alisema alisema amemtumia ujumbe mfupi kuwa anahitajika makao makuu  ya polisi mkoa, kwa mahojiano.

“Natangaza kwamba kuanzia leo (jana) tunamsaka, aje kujisalimisha, tunamsaka hata huko aliko tutamkamata haat kama yupo uvunguni mwa kitanda,” alisema.

Alisema ataendelea kujificha ficha hadi lini,  Mkutano wa Bunge unaanza mwezi ujao, Juni 12, “tutamkamata tu na hapo atakuwa amejivunjia heshima yake.”

Bila kuwataja wanachama wengine wanaohojiwa, DCP Mngulu alisema baadhi ya maneno yanayodaiwa kutamkwa ni kama, “endapo polisi hawatawakamata watu waliohusika na mauaji ya mwenyekiti wa Chadema tawi la Usa River, wilayani Arumeru,  Msafiri Mmbwambo, basi watajitangazia uhuru eneo la Meru pamoja na mikoa ya kaskazini kwa kushirikiana na baadhi ya mikoa ya Kanda ya ziwa.”

Pia alisema walitamka kwamba wanampiga marufuku Rais na Waziri Mkuu kutembelea Mkoa wa Arusha maneno ambayo sio mazuri na baadhi ya waliohusika wamewasiliana nao.

Hata hivyo, hakuwataja watu watatu wanaoshikiliwa kwa mahojiano, lakini habari zilizopatikana eneo la polisi ziliwataja watu hao kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), John Heche, aliyekuwa diwani wa Kata ya Sombetini  kabla ya kuhamia Chadema, Alphonce Mawazo na mwanachama wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Arusha, kabla ya kuhamia Chadema, Ally Bananga.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles