Wednesday May 4, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Lukuvi: Hatuna takwimu za vifo kwa `Babu`

8th May 2012
Print
Comments
Babu wa Loliondo, Mchungaji Ambilikile Mwasapile

Serikali imesema haina takwimu sahihi za vifo vya wagonjwa waliopoteza maisha kutokana na kukatisha dawa za kurefusha maisha baada ya kunywa kikombe cha Babu wa Loliondo, Mchungaji Ambilikile Mwasapile, na haijui alipo kwa sasa.

Mchungaji huyo kuanzia mwishoni mwa mwaka juzi na mwanzoni mwa mwaka jana alikuwa akitoa dawa ya miti shamba ambayo alidai inaponya magonjwa sugu ukiwemo Ukimwi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, jana alisema serikali haina taarifa za mchungaji huyo wala haijui takwimu sahihi za vifo vya wagonjwa walioacha dawa ya kurefusha  maisha ARVs baada ya kupata kikombe.

Lukuvi aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, baada ya kufungua warsha ya viongozi wa dini na viongozi wa vyama vya siasa kuhusu mbinu za kupambana na ugonjwa wa Ukimwi.

“Ni kweli serikali ilikuwa inajua taarifa za mchungaji huyo, lakini kwa sasa haijui yupo wapi na anafanya nini labda waulizwe viongozi wake wa dini,” alisema.

Lukuvi alisema watu walioacha dawa ya kurefusha maisha baada ya kunywa kikombe walifanya makosa makubwa na kukiri kuwa wengi wao wameshapoteza maisha.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles