Tuesday May 3, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

JWTZ kuwadhibiti walioghushi vyeti

16th May 2012
Print
Comments

Jeshi la Ulinzi la Wananchi Watanzania (JWTZ), limeanza kufanyia kazi taarifa zilizotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) za kuwepo kwa wanajeshi 248 walioghushi vyeti vya elimu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe, alisema jeshi hilo kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwemo Nida, watashirikiana katika kufanya uchunguzi huo ili wahusika watakaobainika wachukuliwe hatua kwa mujibu wa kanuni za majeshi.

“Kanuni za majeshi ya ulinzi (Defence Force Regulation), aya ya 8.26. (1) ©  zinaeleza kuwa mwanajeshi anayegundulika kudanganya katika taarifa anazotoa wakati wa kujiunga na jeshi atashitakiwa katika Mahakama za kijeshi na akipatikana na hatia anapewa adhabu kali zinazoambatana na kufukuzwa kazi,” alisema.

Hata hivyo, Kanali Mgawe alisema bado ni mapema sana kuthibitisha ukweli wa taarifa hizo, kwa kuwa zinaweza kuwa za ukweli au laa.

“JWTZ lingependa kueleza kuwa ni mapema mno kwa hivi sasa kuthibitisha ukweli wa taarifa hizo kwa kuwa zinaweza kuwa za kweli au zisiwe za ukweli,” alisema.

Taarifa za kuwepo kwa kashfa ya baadhi ya wanajeshi kughushi vyeti vyao, zilitolewa juzi na Mkurugenzi Mkuu wa Nida, Dickson Maimu, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, ambaye alisema wanajeshi waliobainika ni 248 na polisi ni 700.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles