Friday May 24, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Bweni la wanafunzi lateketea kwa moto

24th July 2012
Print
Comments

Bweni la wavulana katika Shule ya Sekondari  Ulete Wilaya ya Iringa Vijijini, limeteketea kwa moto pamoja na mali mbalimbali za wanafunzi zenye thamani ya Sh. 6,398,0000.

Kamanda wa Polisi mkoani Iringa, Michael  Kamuhanda, alisema moto huo ulizuka Julai 20, mwaka huu saa 3:30 asubuhi wakati wanafunzi wakiwa darasani.

Alisema watu wasiofahamika waliwasha moto huo na sababu za kufanya hivyo bado hazijafahamika.

Hata hivyo, alisema hakuna anayeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo na polisi wanaendelea na uchunguzi.

 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment