Wednesday May 4, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Jerry Rawlings ausifia upinzani nchini

8th May 2012
Print
Comments
Rais Mstaafu wa Ghana, Jerry Rawlings

Rais Mstaafu wa Ghana, Jerry Rawlings, amevisifu vyama vya upinzani nchini, kwa  kuwa vimefanya makubwa kwa kuibana serikali, jambo lililopelekea  serikali kufanya mabadiliko ya baraza la mawaziri.

Alikuwa akizungumza Jijini Dar es Salaam jana kwenye Mkutano wa sita wa  Chama Cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA), unaowakutanisha Viongozi wa Vyama vya Siasa,  pamoja wabunge wa nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Shelisheli, Rwanda, na  Burundi.

Mkutano huo wa siku tatu unalengo  la kuangalia nafasi, haki, wajibu  wa  upinzani na serikali katika maendeleo ya nchi, Rawlings alisema kazi inayofanywa na upinzani hapa nchini inapendeza na inapaswa kuigwa.

“Kilichofanywa na upinzani ni jambo la kuigwa na ndiyo kazi ya upinzani kukosoa na kuibana serikali ili iweze kufanya mabadiliko pale inapoonekana kuwa mambo hayaendi sawa,” alisema.

Aidha, Rawlings alibainisha kuwa Serikali nyingi za nchi za kiafrika zina tabia ya kutumia nguvu pale zinapotaka kupitisha au kufanya mambo yake, na kuasa kuwa ni wakati mwafaka sasa kwa upinzani kuwa macho na tabia hizo, ili kuruhusu utamaduni wa kweli wa demokrasia.

Akizungumzia mapinduzi ya kijeshi kwenye nchi ya Mali na Guinea Bissau, Rawlings alisema kuwa kinachotokea kwenye nchi hizo inaonyesha kuwa kuna tatizo kubwa la kidemokrasia, na kuwepo kwa mfumo mbovu.

Aliongeza kuwa demokrasi ni muhimu sana kwa binadamu, kwani unaweza kumpa kila kitu, lakini kama mtu huyo hana uhuru wa kujieleza na kutoa maoni yake ni kazi bure, huku akitoa mfano wa Libya.

“Yanayotokea Tripoli, ingawa ni tofauti kidogo, lakini inaonyesha kuwa pamoja na kupewa kila kitu, lakini wananchi hawakuridhika, ni kama vile maandiko yanayosema mtu hataishi kwa mkate tu, kwani maisha ni zaidi ya mkate,” alisema.

Naye Spika wa Bunge, Anne Makinda katika hotuba yake iliyosomwa na Mwenyekiti wa Bunge, Sylivester Mabumba, aliosema moja ya mafanikio makubwa ya Bunge la sasa ni kuwepo kwa wapinzani ambao wanaongoza kamati tatu tofauti za Bunge ambazo ya ni  Hesabu za Serikali (PAC), Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC).

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles