Friday Apr 29, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

JK: Serikali italinda ardhi ya wakulima wadogo

10th May 2012
Print
Comments
Rais Jakaya Kikwete,(wa 2kulia) na viongozi wenzie wa Afrika wakiwa katika mdahalo wa taasisi ya kilimo ya GroAfrica kwenye jengo la Makao Makuu Mapya ya Umoja wa Afrika (AU)jijini Addis Ababa, Ethiopia jana. Kutoka kushoto ni Rais Mstaafu wa Nigeria, Olusegon Obasanjo, Rais wa Rwanda, Paul Kagame na Rais wa Ethiopia, Meles Zenawi.

Rais Jakaya Kikwete amesema  kuwa miradi mikubwa ya kilimo ya kibiashara nchini itatekelezwa kwa shabaha mbili kubwa, kuwatoa wakulima katika umasikini na kulinda miliki ya ardhi yao.

Pia alisema kuwa Mradi wa Uendelezaji Kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania – Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania (SAGCOT) unakuwa ni mfano unaong’ara wa uendelezaji kilimo katika Bara la Afrika.

Akizungumza na Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), Dkt. Rajiv Shah kwenye Hoteli ya Sheraton mjini Addis Ababa, Ethiopia jana, Rais Kikwete alisema kuwa shabaha kuu ya miradi kama SAGCOT ni kuwatoa wakulima wa Tanzania katika umasikini katika kipindi kifupi na kulinda miliki ya ardhi yao.

Rais Kikwete na Dk. Shah wako mjini Addis Ababa, Ethiopia kuhudhuria Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF), Kanda ya Afrika, ulioanza jana.

Rais alisema kuwa wakulima wakubwa watapewa ardhi tu pale ambako iko ardhi ya kutosha na hata baada ya kupewa ardhi watatakiwa kuwasaidia wakulima wadogo wanaokuwa wanaishi jirani na shamba la wakulima hao wakubwa.

“Tutawapa ardhi kubwa wakulima wakubwa pale ambako iko ardhi ya kutosha. Na hata baada ya kuwa tumepewa ardhi hiyo,  wakulima hao wakubwa watatakiwa kuwasaidia na kushirikiana na wakulima wadogo.

Hii ndiyo namna pekee ya kuwasaidia wakulima wetu kuondokana na umasikini,” alisema Rais Kikwete.

Naye Dk. Shah alimwambia Rais Kikwete kuwa Marekani imedhamiria kuhakikisha kuwa SAGCOT unakuwa miradi wa mfano unaong’aa Afrika. USAID ni moja ya mashirika ya kimataifa ambayo inashirikiana na Serikali katika kuendeleza mradi huo.

Katika mkutano mwingine, Mtendaji Mkuu wa Benki ya HSBC, Andrew Dell, alimwambia Rais Kikwete kuwa benki yake iko tayari kuiwezesha Tanzania kukopa fedha nyingi za ujenzi wa miundombinu kwa mpango wa Sovereign Bond badala ya kutumia fedha za kodi kujenga miundombinu ambayo inaweza kujengwa kwa urahisi na kwa kutumia fedha ya benki hiyo.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles