Saturday May 25, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

`Mauaji ya kimbari yameipaisha Rwanda`

5th April 2012
Print
Comments

Jumuiya ya kimataifa  imetakiwa kuiga mfano wa Rwanda kupitia maendeleo iliyoyapata katika utawala bora baada ya miaka 18 ya  mauaji ya kimbari, kwani zimezidi hata nchi ambazo hazikukumbwa na migogoro.

Rai hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mshauri Mwandamizi wa Ubalozi wa Rwanda nchini, Sano Lambert,  wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu siku ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari itakayofanyika keshokutwa.

Lambert alisema baada ya mauaji ya kimbari nchi hiyo ilipokea maoni mbalimbali yanayohusu amani na maendeleo ya uchumi na imeyafanyia kazi, hivyo kumbukumbu ya mauaji hayo hufanyika duniani kote ili kuikumbusha jamii umuhimu wa kujifunza kutokana na historia ya nchi hiyo na kutengeneza matumaini mapya kwa kizazi kipya.

Alisema kuwa kumbukumbu ya mauaji hayo ina umuhimu mkubwa katika kuikumbusha jamii ya Rwanda kuhusu vitendo na kauli zao ambazo zinaweza kuleta mauaji mengine na kujitahidi kuzizuia.

Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa  (UNIC), Stella Vuzo, alisema kuwa maadhimisho ya kumbukumbu ya mauaji ya Rwanda yameleta  athari kubwa ulimwenguni.

“Uelewa wa watu kwenye nchi tofauti juu ya mauaji ya kimbari yamesababisha kuibuka kwa taasisi nyingi zinazojihusisha na haki za binadamu na kuamsha shughuli nyingi zinazojihusisha na masuala ya haki za binadamu,” alisema Vuzo.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment