Friday May 6, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

TRL yakataliwa kupandisha nauli

11th May 2012
Print
Comments
Katibu Mtendaji Baraza la Sumatra, Osca Kikoyo

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi kavu na Majini (Sumatra), imekataa maombi la Kampuni ya Reli Tanzania (TRL),  kutaka kupandisha nauli ya treni za reli ya kati na kulitaka shirika hilo kuboresha huduma kwanza.

Akikataa pendekezo hilo lililowasilishwa na TRL kutaka kuongezeka kwa viwango vya nauli kwa asilimia 25 kwa wasafiri wa daraja la kwanza na la pili  pamoja na  asilimia 50 kwa daraja la tatu, Katibu Mtendaji Baraza la Sumatra, Osca Kikoyo, alisema watumiaji wa huduma za TRL ni watu wenye kipato cha chini.

Kikoyo alisema, ongezeko la nauli kwa sasa linaweza kuwahamishia abiria  kwenye mabasi kwa sababu barabara zinazidi kuboreshwa hivyo kupelekea kukimbia usafiri wa treni.

“Takwimu zinaonyesha abilia walipungua tangu ongezeko la nauli la mwaka 2009 kwani idadi ilipungua kutoka 548,819 hadi 290.046 kwa mwaka 2010,” alisema Kikoyo.

Alisema ongezeko la asilimia 50 kwa wakati mmoja ni kubwa sana ukilinganisha na huduma zinazotolewa na shirika hilo, hivyo wanapaswa kuboresha kwanza huduma kuliko kukimbilia kupandisha nauli

“Huduma zinazotolewa na TRL ni mbaya na hazina uhakika, hivyo yawapasa kuziboresha, na ongezeko la nauli za abiria haliwezi kulikwamua TRL kwa sababu mchango wake ni mdogo mno,” alisema Kikoyo.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles