Thursday May 23, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Uchaguzi Naibu Meya Arusha washindikana

23rd July 2012
Print
Comments

Uchaguzi wa Naibu Meya Halmashauri ya Manispaa ya Arusha  uliokuwa ufanyike mwishoni mwa wiki iliyopita umeshindikana, baada ya  Madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kususia kikao na kukacha kupeleka jina la mgombea wake.

Awali, akifungua kikao hicho, Meya wa Manispaa hiyo, Gaudence Lyimo, alisema kikao hicho kilikuwa na ajenda kubwa mbili.

Alisema ajenda ya kwanza ilikuwa ni kufanya uchaguzi wa Naibu Meya ambaye alitakiwa kutoka Chadema, lakini chama hicho hakikupeleka jina wala madiwani wake kuhudhuria.

Alisema kitendo hicho kimesababisha kikao hicho kusogezwa mbele mpaka hapo kitakapoitishwa kingine cha dharura kujadili suala hilo.

“Hapa waheshimiwa madiwani kikao hiki kilitakiwa kuwa na washirikia 23 ambao kati yao watano ni wabunge ambao wapo bungeni na 18 ni madiwani, ila hapa wapo madiwani 12 tumefika nusu ya kolamu ila Chadema wameandika barua na kueleza sababu zao za kususia kikao hiki  kuwa wanataka uchaguzi wa Meya ufanyike tena na kuitaka serikali kufanya hivyo, ndipo wao washiriki,” alisema.

Lyimo alisema anakishangaa chama hicho kwa hatua yake hiyo, kwani kama kinaona hakitendewi kuna sehemu ya kukimbilia ambako ni mahakamani.

Alisema Juni 20 mwaka jana kilifanyika kikao cha pande hizo mbili na kukubaliana muafaka wa kutoa nafasi ya Naibu Meya kwa Chadema, lakini baada ya muda madiwani waliokubali muafaka huo walifukuzwa.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment